Ziwa Chilwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ziwa Chilwa
seen from space (false color)
Mahali Wilaya ya Zomba
Mito ya kuingia Naisi, Thondwe, Phalombe, Songani, Domasi
Mito ya kutoka (hakuna)
Nchi za beseni Malawi
Urefu km 60
Upana km 40
Visiwa Chisi
Ziwa Chilwa jinsi linavyoonekana kutoka angani.

Ziwa Chilwa ni ziwa la pili kwa ukubwa nchini Malawi, baada ya Ziwa Nyasa. Liko kwenye wilaya ya Zomba, karibu na mpaka wa Msumbiji.

Urefu wake ni km 60, upana ni km 40. Katikati ya ziwa hilo kuna kisiwa kiitwacho Chisi. Hakuna mto unaotoka katika ziwa.

Wakazi wa vijiji 335 karibu na Ziwa Chilwa[1] huvua samaki hapa; zao lote ni takriban tani 17,000 kwa mwaka.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kalinga, Owen J. M. (2012-01-01). Historical Dictionary of Malawi (in en). Rowman & Littlefield. ISBN 9780810859616. 
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Chilwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.