Nenda kwa yaliyomo

Yerry Mina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yerry Mina.

Yerry Fernando Mina González (alizaliwa Septemba 23, 1994) ni mchezaji wa soka wa Colombia ambaye anacheza kama beki wa kati wa klabu ya Hispania FC Barcelona.

Mnamo tarehe 11 Januari 2018, FC Barcelona na Palmeiras walifikia makubaliano ya uhamisho wa Yerry Mina kwa mkataba wa miaka mitano hadi 30 Juni 2023. Hii ilimfanya Mina kuwa Mkolombia wa kwanza kuchezea FC Barcelona. Gharama ya uhamisho ilikuwa £ milioni 11.8.

Mina alichukuchukua nafasi ya Gerard Pique katika dakika ya 83 ya mchezo wa Copa del Rey dhidi ya Valencia, Barcelona ilishinda 2-0.Alifanya mchango wake wa kwanza katika klabu kumsaidia Ousmane Dembélé katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Villareal.

Mnamo Mei 2018 aliitwa katika kikosi cha kwanza cha Kolombia kwa ajili ya Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yerry Mina kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.