Nenda kwa yaliyomo

Xenofoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Xenophon)
Xenofoni, mwanahistoria wa Ugiriki

Xenofoni (pia Xenophon; mnamo 430 KK354 KK) alikuwa mwanahistoria, askari na mwanafalsafa wa Ugiriki ya Kale aliyeishi wakati mmoja na Sokrates. Anajulikana kwa maandishi yake juu ya historia ya nyakati zake mwenyewe yaani karne ya 4 KK. Alihifadhi pia maneno ya Sokrates[1], na maelezo ya maisha katika Ugiriki ya Kale na Milki ya Uajemi.

Alikuwa kiongozi wa jeshi la Wagiriki walioajiriwa na mdogo wa mfalme wa Uajemi aliyejaribu kumpindua kaka yake; Xenofoni aliwaongoza Wagiriki hadi Babeli na baada ya kifo cha mwajiri wao aliwaongoza pia kwenye safari ya kurudi.[2]

Maandiko yake mashuhuri ni pamoja na

  • Anabasis, anaposimulia historia ya mamluki Wagiriki 10,000 wakirudi kwao baada ya kuajiriwa kwa mapigano kati ya viongozi wa Kiajemi; Xenofoni mwenyewe aliwahi kuongoza safari hii.
  • Hellenika, ambayo ni historia ya Ugiriki kati ya mwaka 411 KK hadi 362 KK
  1. "An Introduction to the Work of Xenohon". Xenophon (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-08-24.
  2. Ambler, Wayne (2011). The Anabasis of Cyrus. Translator's preface: Cornell University Press. ISBN 978-0-8014-6236-8.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Marejeo katika mtandao