Wilaya ya Masasi
Wilaya ya Masasi ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Mtwara. Maeneo ya mji wa Masasi yalikuwa sehemu ya wilaya hii lakini tangu mwaka 2011 mji ulipata halmashauri yake kwa hiyo kama wilaya ya pekee.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 247,993 [1]
Masasi ni wilaya kubwa ya Mtwara; inapakana na Mkoa wa Lindi upande wa kaskazini, Mkoa wa Ruvuma upande wa magharibi na nchi ya Msumbiji upande wa kusini. Upande wa mashariki kuna mpaka na wilaya ya Newala.
Eneo la wilaya ni 4,429 km² linajumlisha asilimia 23 ya eneo lote la Mkoa wa Mtwara.
Kuna majimbo ya uchaguzi wa bunge mawili ambayo ni Lulindi na Masasi.
Vitengo vya chini ni tarafa 5, kata 22, vijiji 170 na vitongoji 986.[2].
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Wakazi walio wengi ni wakulima wadogo. Zao la biashara ni hasa korosho lenye soko zuri na mapato ya wakazi ni wastani TSHs 720,000 kila mmoja kwa mwaka 2010/11 [3]. Mazao ya chakula ni pamoja na muhogo, mahindi, mpunga, mboga majani na matunda. Wengine hufuga mbuzi, ng'ombe, nguruwe na kuku.
Hakuna tasnia.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Sensa ya 2012, Mtwara region - Masasi District Council
- ↑ [Masasi Revenue study Report, uk 4 - idadi ya kata ilitajwa hapo kuwa 34, imesahihishwa hapa kulingana na sensa ya 2012 Ilihifadhiwa 4 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Ling. Masasi Revenue Study Report, mwaka 2011
Kata za Wilaya ya Masasi Vijijini - Tanzania | ||
---|---|---|
Chigugu | Chikoropola | Chikukwe | Chikundi | Chikunja | Chiungutwa | Chiwale | Chiwata | Lipumburu | Lukuledi | Lulindi | Lupaso | Makong'onda | Mbuyuni | Mchauru | Mijelejele | Mitesa | Mkululu | Mlingula | Mnavira | Mpanyani | Mpeta | Mpindimbi | Msikisi | Mwena | Namajani | Namalenga | Namatutwe | Namwanga | Nanganga | Nangoo | Nanjota | Ndanda | Sindano |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mtwara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Masasi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |