Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala ya wiki/Virusi vya corona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Virusi vya corona

Virusi vya Corona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ni kundi la virusi vinavyoweza kusababisha magonjwa kwa wanyama (mamalia na ndege) lakini pia kwa binadamu. Inaaminiwa ni aina ya virusi vilivyohama kutoka kwa wanyama na kuathiri binadamu pia.

Covid-19 (2019 Novel Coronavirus)

Mwisho wa mwaka 2019 lilitokea badiliko jipya la virusi vya corona lililotambuliwa mara ya kwanza mjini Wuhan, China. Wagonjwa walionyesha matatizo kwenye njia ya upumuaji; wengine waliathiriwa kidogo tu, lakini wengine waliugua vibaya hadi kufa. Dalili zilizotambuliwa hadi mwisho wa Januari 2020 ni pamoja na homa, kukohoa na ugumu wa kuvuta pumzi.

  • zaidi ya asilimia 80 za wagonjwa huonekana kuwa na ugonjwa mwepesi, wanapona
  • kati ya asilimia za wagonjwa kuna maambukizi mazito yanayosababisha matatizo ya kupumua, hata nimonia.
  • takriban asilimia 5 huwa na magonjwa hatari
  • mnamo asilimia 2 hufa; hatari ya kifo inapatikana hasa kwa wazee, kuna mfano michache ya watoto ►Soma zaidi