Wikipedia:Makala ya wiki/Kupatwa kwa Mwezi
Mandhari
Kupatwa kwa Mwezi (kwa Kiingereza: lunar eclipse) ni hali ya Mwezi kutoonekana kwa sehemu au kabisa kwa muda hadi kuonekana tena kama mwezi mpevu. Badiliko hili linaweza kudumu saa moja hadi nne. Hali inayopelekea kupatwa kwa mwezi kunasababishwa na kivuli cha Dunia kinachomwaga giza juu ya Mwezi kabisa au kwa sehemu. Hali hii inatokea wakati Mwezi - Dunia na Jua zinakaa katika mstari mmoja, Dunia ikiwa katikati ya Jua na Mwezi. Hapo kivuli cha Dunia inafunika Mwezi. Inatokea tu wakati wa mwezi mpevu. ►Soma zaidi