Who Am I?
Who Am I? | |
---|---|
Imeongozwa na | Benny Chan Jackie Chan |
Imetayarishwa na | Leonard Ho Barbie Tung |
Imetungwa na | Jackie Chan Susan Chan Lee Reynolds |
Nyota | Jackie Chan Michelle Ferre Yamamoto Mirai Ron Smerczak Ed Nelson Washington Xisolo |
Muziki na | Nathan Wang |
Imehaririwa na | Peter Cheung Yau Chi Wai |
Imesambazwa na | Golden Harvest Columbia Pictures (US na Ufalme wa Muungano) |
Imetolewa tar. | Hong Kong 17 Januari 1998 |
Ina muda wa dk. | Hong Kong: 120 mins. USA: 107 mins |
Nchi | Hong Kong |
Lugha | English Cantonese |
Mapato yote ya filamu | HK$38,852,845 |
Who Am I? ((Kichina)) ni filamu ya Hong Kong ya kupigana iliyotolewa na Golden Harvest. Iliongozwa na Jackie Chan, ambaye pia aliigiza kama muhusika mkuu na pia alitumbuiza wimbo wa kumalizia katika filamu hiyo.
Katika mataifa mengine filamu hii pia inajulikana kwa majina yafuatayo:
- Jackie Chan's Who Am I? (USA)
- Amnesia (Norway)
- Jackie Chan Is Nobody (Germany)
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Mwanachama wa kikosi cha kimataifa kilichoungwa mkono na CIA cha ‘’black ops special force’’ ako katika misheni ya kuwateka nyara wanasayansi wa afrika Kusini wanaoendelea kutayarisha sumu kali inayoletwa duniani na ‘’meteorite’’. Kulingana na data ya tarakilishi inayoonyesha majina ya wahusika katika mradi huo, mmoja wao ni ‘Jackie Chan’ (Chan). Anaangukia katika tukio lililopangwa ambalo linasababisha kifo cha wenziwe. Anaponea lakini anaangukia katika veldt ya Afrika na amepoteza kumbukumbu yake ya matukio ya awali. Anapoulizwa na wenyeji kuhusu jina lake anajibu, “Mimi ni Nani?” ‘’(Who Am I?)’’ ambalo wanachukulia kuwa jina lake. Anaanza kupokea visengere nyuma (flashbacks) ambavyo vinaashiria hati halisi ya 'Who am I?'. Anaanza urafiki na wanawake wawili: Christine (Michelle Ferre), ambaye ni ajenti wa CIA anayefanya kazi kisiri akijisitiri chini ya hati ya uandishi wa habari, na Yuki (Yamamoto Mirai).
Waliokuwa maafisa wa Jeshila US wa Renegade pamoja na wauzaji silaha wa ‘’black market’’ wanauza sumu hiyo nje za nchi kinyume cha sheria na 'Who am I?' ndiye tishio la pekee la biashara yao. Maajenti wanatumwa nje kumzuia 'Who am I?' asizifichue shughuli zao za kiharifu. Anawashinda wengi waliokuwa wanajeshi la Renegade na anajiingiza katika pigano kali na la hatari juu ya baa la nyumba mjini Rotterdam dhidi ya wapiganaji wawili bora zaidi wa Morgan, huku akifanya sarakasi ambayo imetumiwa kama signature ya filamu na kuwaangusha kutoka baa hilo la vioo. CIA inawatia nguvuni na 'Who am I?' anakumbuka hati yake halisi.
Vidokezo vya Utoaji
[hariri | hariri chanzo]- Filamu hii ilitengenezwa kati ya Februari na Machi 1997.
- Wakati wa sehemu katika filamu hiyo, kuna habari katika matangazo ya Posta kuhusu maumbile ya Chan anayetafutwa, ikitaja urefu wake kama 5'10". Urefu wake halisi ni 5'8".
- Filamu hii inaonyesha moja kati ya maonyesho makubwa zaidi ya mafukuzano ya magari kwa Chan, huku akitumia gari lake la Mitsubishi Lancer Evolution IV.
- Mhusika Chan anaishi chumba nambari 1954 cha Hotel. 1954 ndio mwaka wa kuzaliwa wa Chan.
- Filamu hii inashirikisha meneo mengi ya Rotterdam kama vile Erasmus Bridge, Beurstraverse (ambayo ilitumiwa kama Johannesburg), Cube Houses na Jengo la Willemswerf.
Matoleo ya DVD
[hariri | hariri chanzo]Toleo la DVD ya US limepunguzwa kwa dakika 9 kufuatilia mabadiliko na kurukwa kwa sehemu zifuatazo:
- Sehemu ambapo kikosi cha 'Who am I?’ kinarukwa maradufu kinaonekana kama kirejeshi katikati ya Filamu. Katika toleo la US sehemu hiyo inaonekana punde baada ya Jackie Chan kumaliza misheni yake.
- Majadiliano kati ya 'Who am I?' na jamii ya Kiafrika yamekatwa kwa ustadi mkubwa, huku baadhi ya sehemu zilitolewa
- sehemu ya mbio za magari imefupishwa.
- Sehemu ambapo 'Who am I?’ anapata hisia zake za mdomo na kusimulia hali yake kwa Yuki imekatwa.
- Marudio yote ya papo hapo katika filamu isipokuwa mawili yamefutwa.
Box office
[hariri | hariri chanzo]Who Am I? ilipata mauzo ya mwaka ya HK $38,852,845 katika maonyesho yake nchini Hong Kong
Tuzo na Uteuzi
[hariri | hariri chanzo]- 1999 Hong Kong Film Awards
- Mshindi: Koreografia ya kupigana bora zaidi (Jackie Chan)
- Nomination: Mwigizaji Bora Zaidi (Jackie Chan)
- Nomination: Uhariri bora zaidi wa filamu (Peter Cheung, Chi Wai Yau)
- Nomination: Picha Bora zaidi (Barbie Tung) (executive producer)
- Nomination: mundo bora zaidi wa Sauti
Tazama Pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Who Am I? at the Internet Movie Database
- (Kiingereza) Who Am I? katika Allmovie
- Who Am I? Ilihifadhiwa 14 Oktoba 2019 kwenye Wayback Machine. related article PodcastOnFire.com Ilihifadhiwa 14 Oktoba 2019 kwenye Wayback Machine.