Waris Dirie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Waris Dirie

Waris Dirie (kwa Kisomali: Waris Diiriye; alizaliwa nchini Somalia mnamo mwaka 1965) ni mwandishi, mwigizaji na mwanaharakati wa haki za binadamu katika kupambana na ukeketaji (FGM). Waris kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2003 alikuwa balozi maalum wa Umoja wa Mataifa dhidi ya masuala ya ukeketaji kwa wanawake. Mwaka 2002 alianzisha shirika huko Vienna la Foundation Flower Foundation.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Dirie ni mmoja kati ya watoto kumi na wawili katika familia ya wahamaji katika eneo la Galkayo. Jina lake la kwanza, Waris, linamaanisha maua ya Jangwa. Alipokuwa na umri wa miaka mitano alikeketwa na aliteseka kwa njia ya uharibifu; baadae alipokuwa na umri wa miaka 13 alikimbilia jangwani kuelekea Mogadishu ili kuepuka ndoa iliyopangwa afunge na mtu mwenye umri wa miaka 60.

Miongoni mwa ndugu zake ambaye alikuwa Balozi wa Somalia nchini Uingereza wakati huo alikuwa akitafuta mjakazi. Lakini kwa msaada wa shangazi yake alimshawishi mjomba wake kuajiri na kumpeleka London ambako alifanya kazi katika nyumba ya mjomba wake kwa kulipa gharama kidogo. Dirie aliondoka kwa mjomba wake akaishi katika makazi yasiyo ya uhakika, baadaye akakodi chumba.[1][2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Stellan Consult Limited (2008). "Desert Flower". Parents (ref 265–270): 76. 
  2. Mary Zeiss Stange, Carol K. Oyster, Jane E. Sloan, ed. (2011). Encyclopedia of Women in Today's World, Volume 1. SAGE. uk. 402. ISBN 1412976855. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waris Dirie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.