Chama cha kisiasa
Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani faida zao za binafsi.
Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao.
Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.
Penye mfumo wa chama kimoja kazi ya chama itakuwa tofauti. Historia ina mifano ya kwamba chama pekee kinaelekea kwenye udikteta kwa viwango tofauti.
Vyama hutofautiana sana kuhusu kiasi cha tofauti za maoni zinazoruhusiwa ndani yao, uhusiano kati ya viongozi na wanachama, kiasi cha uwezo wa wanachama kuathiri mwelekeo wa chama na umuhimu wa programu.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |