Volta (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Tawimito ya Volta ndiyo Muhun (Volta nyeusi), Nazinon (Volta nyekundu) na Nakambe (Volta nyeupe) pamoja na maungano ya mito katika Burkina Faso na Ghana


Mto wa Volta
Mto Volta kusini ya lambo la Akosombo
Chanzo maungano ya mito ya Muhun, Nazinon na Nakambe karibu na mji wa Salaga (Ghana)
Mdomo Bahari ya Atlantiki
Nchi Ghana
Urefu 2,574 km pamoja na tawimto wa Muhun (Volta Nyeusi)
Kimo cha chanzo 180 m kwenye maungano ya mito
Tawimito Muhun, Nazinon na Nakambe

Volta ni mto muhimu wa Afrika ya Magharibi. Inaanza katika maungano ya tawimito yake ya Muhun (Volta nyeusi), Nazinon (Volta nyekundu) na Nakambe (Volta nyeupe) karibu na mji wa Salaga / Ghana.

Katika Ghana boma la lambo la Akosombo (Ghana) limesababisha kutokea kwa ziwa la Volta ambalo ni lambo kubwa kabisa duniani. Baada ya kuondoka katika ziwa hili lisilo asilia Volta inaingia katika Ghuba ya Guinea ya bahari Atlantiki.