Vince Hayes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vince Hayes

James Vincent Hayes (anajulikana pia kama Vic Hayes; 24 Machi 1879 - 1 Juni 1964) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu aliyejiunga na timu ya mpira ya Newton Heath mnamo Februari mwaka 1901. Katika timu ya Newton Heath, ambayo ilipewa jina la Manchester United mnamo mwaka 1902, alipata majeraha kadhaa. Alivunjika miguu yote mnamo mwaka 1905, na muda mfupi baada ya kupona, akavunjika tena. Aliondoka United kwenda Brentford FC. mnamo Mei mwaka 1907, lakini alirudi tena United mnamo Juni mwaka 1908.[1] Aliisaidia klabu kushinda Kombe la FA la mwaka 1909.[2].Aliondoka Manchester United mnamo Novemba 1910 baada ya kufunga magoli mawili katika mechi 128 alizocheza.[3]

Baadae alifanikiwa kuwa kocha wa Norway mnamo mwaka 1912 katika mashindano ya Olympics,na pia akawa kocha wa Wiener SC.Mnamo mwaka 1923.Aliteuliwa kuwa msimamizi wa mwisho katika timu ya Atlético Madrid iliyopo Hispania

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. White, Eric, mhariri (1989). 100 Years Of Brentford. Brentford FC. uk. 359. ISBN 0951526200. 
  2. "Manchester United 1 Bristol City 0". FA-CupFinals.co.uk. Retrieved 19 March 2013.
  3. Hayes. Manchester United. Retrieved 19 March 2013.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vince Hayes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.