Nenda kwa yaliyomo

Valentin Nouma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Valentin Nouma
Picha ya Valentin Nouma

Valentin Nouma ni mchezaji wa soka kutoka nchini Burkina Faso, ambaye alizaliwa tarehe 14 Februari mwaka 2000 jijini Bobo-Dioulasso. Ana uraia wa Burkina Faso na anacheza nafasi ya beki wa kushoto[1].

Nouma alianza kazi yake ya soka na Rahimo FC, ambapo alianza kujitaftia umaharufu wake katika Ligi Kuu ya Burkina Faso. Alijiunga na AS Douanes ya Senegal na baadaye kucheza katika klabu ya Saint Eloi Lupopo ya DR Congo.

Mwaka 2024, Nouma alihamia Simba S.C. iliyopo Tanzania baada ya mkataba wake na Saint Eloi Lupopo kumalizika. Uhamisho huu unatarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi ya Simba SC.

Nouma pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Burkina Faso, akiwa amecheza mechi sita tangu aanze kucheza kimataifa mwaka 2018[2].

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Valentin Nouma kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.