Uwanja wa michezo wa Mashahidi wa Pentekoste

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Mashahidi wa Pentekoste.

Uwanja wa Mashahidi wa Pentekoste (kwa Kifaransa: Stade des Martyrs de la Pentecôte, pia unajulikana kama Stade Kamanyola) ni uwanja uliopo Lingwala huko Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Unatumika hasa kwa mechi za mpira wa miguu, matamasha,na mashindano ya riadha.

Ni uwanja wa nyumbani wa Timu ya Kitaifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, AS Vita Club na DC Motema Pembe wa Championship Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Uwanja una uwezo wa kuchukua watu 80,000 kwa mechi za kimataifa, lakini uwezo wake ni watu 125,000 kwa mechi nyingine.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Stade des Martyrs hapo awali uliitwa Stade Kamanyola. Ujenzi ulianza Oktoba 14, 1988 na kumalizika Oktoba 14, 1993.

Mnamo 1997, uwanja huo ulipewa jina jipya la "Stade des Martyrs de la Pentecôte" ikiwa ni kumbukumbu ya mawaziri wanne waliofukuzwa na Mobutu Sese Seko na kunyongwa katika uwanja huo tarehe 2 Juni 1966; mawaziri hao ni Évariste Kimba, Jérôme Anany, Emmanuel Bamba, na Alexandre Mahamba.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Mashahidi wa Pentekoste kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.