Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa michezo wa Fez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa michezo wa Fez

Uwanja wa michezo wa Fez ni uwanja wa michezo wenye matumizi mengi unaopatikana Fez,Moroko. Unatumika sana kwa michezo ya soka na riadha. Uwanja huu una uwezo wa kubeba mashabiki 45,000(Elfu arobaini na tano) na ulijengwa mwaka 2003.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya uwanja huu ulichorwa na wasanifu na wahandisi wa Moroko na uzinduzi wa kazi ulifanywa mnamo 1992, lakini ni miaka 2 tu baadaye ndipo ilipoanza ujenzi wake ambao ulilazimika kumalizika mnamo 1997 kwa heshima ya Meknes, Kombe la Mataifa ya Vijana barani Afrika la 1997 lililoandaliwa na Moroko. Uwanja haukumalizika kwa wakati, haswa kwa sababu ya shida za kiufundi, na ilikuwa hadi 2003 ambapo kazi ilikamilishwa.

Ndani ya uwanja kuna chumba cha habari, kituo cha huduma ya kwanza, chumba cha wagonjwa na chumba cha kudhibiti madawa ya kulevya, eneo la kuegesha magari yenye uwezo wa kubeba hadi magari 7500(Elfu saba na mia tano).

Uwanja huu pia uliingia kwenye shindano la kugombea kwa Moroko uandaaji wa kombe la dunia la mpira wa miguu mnamo 2006 na 2010. Katika hafla hii uwanja huo ulikarabatiwa na ulifanyiwa marekebisho kwa kuongeza ujazo wa viti 5000 na uwezo wake wote uliongezeka hadi viti 45000. Lakini mnamo 15 Mei 2004 Afrika Kusini walipewa kuandaa kombe la dunia kwa kura 14 dhidi ya 10 za Moroko.

Uwanja wa Fès ulizinduliwa rasmi tarehe 25 Novemba 2007, miaka minne baada ya kukamilika kwa fainali za Kombe la Enzi la 2006-07 kwa mechi kati ya FAR Rabat (D1) na Rachad Bernoussi (D2), ambayo ilimalizika kwa ushindi wa FAR Rabat ( 1-1, tabs 5 hadi 3). Hapakuwa na kiingilio na watazamaji 40,000 kutoka miji tofautitofauti ya Moroko walihudhuria. Bao la kwanza lililofungwa katika uwanja huu ni bao la Atik Chihab (FAR Rabat).

Tangu kuzinduliwa kwa uwanja huu, timu ya Maghreb ya Fez wamehamishia makazi yao hapo, na ilicheza mechi yake ya kwanza katika uwanja huu, wakati wa mechi ya ligi dhidi ya Vijana wa El Massira. Mechi iliisha kwa sare ya 0-0.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Fez kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.