Uwanja wa michezo wa Dr. Petrus Molemela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo wa Dr. Petrus Molemela[1] ni uwanja wa michezo ambao hapo zamani ulitambulika kama uwanja wa michezo wa Seisa Ramabodu. Ni uwanja wenye matumizi mengi na unapatikana Bloemfontein nchini Afrika Kusini. Kwa sasa unatumika kwa mchezo wa mpira wa miguu na ulitumika kama uwanja wa mazoezi kwa timu zilizoshiriki Kombe la Dunia la FIFA ya mwaka 2010 baada ya kuboreshwa mnamo mwaka 2008 na kufikia viwango vya FIFA.[2]

Ni uwanja wa nyumbani kwa klabu ya Bloemfontein Celtic ambapo hutumia pia uwanja wa michezo wa Free state. Baada ya maboresho ya miaka mitatu(3) iliyokamilika mwaka 2015, uwezo wa uwanja kubeba washabiki uliongezeka kutoka 18,000 hadi 22,000.[3][3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Breathing new life into Mangaung sports (October 23, 2015).
  2. [1]
  3. 3.0 3.1 Guduka, Sidwell. Stadium reopened.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Dr. Petrus Molemela kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.