Uwanja wa michezo wa Obafemi Awolowo
Uwanja wa michezo wa Obafemi Awolowo ni uwanja wa michezo ambao upo katika barabara ya Liberty, Barabara ya Ring huko Ibadan nchini Nigeria, ambao uliitwa Uwanja wa Uhuru hadi mwaka 2010. Ni uwanja wa mpira wa kihistoria wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 25,000.[1]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ujenzi
[hariri | hariri chanzo]Uwanja huo ulifunguliwa mnamo mwaka 1960 wakati wa utawala wa Chifu Obafemi Awolowob ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Mkoa wa Magharibi wakati huo. Uliitwa Uwanja wa Uhuru kwa heshima ya uhuru wa Nigeria.Ulijengwa na wafanyakazi wa moja kwa moja chini ya usimamizi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya mkoa, uwanja huo ulikuwa eneo kuu la michezo katika mkoa wa zamani wa Magharibi mwa Nigeria. Uliwekwa mwishoni mwa Kusini mwa Ibadan mnamo mwaka 1960 karibu na kilele cha kilima, na pia karibu na njia inayopita barabara ya Ibadan-Abeokuta na Ibadan-Lagos.
Ndondi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Agosti 10, mwaka 1963 uwanja huo ulitumika uliandaa pambano la kwanza kabisa la ndondi katika Afrika. Mechi hiyo ilipangwa kuwa Julai 13,mwaka 1963. Hii ilikuwa kwa Mashindano ya Uzito wa Kati wa ukanda wa Dunia na ilipiganwa kati ya wa Nigeria Dick Tiger na Gene Fullmer wa USA.
Kombe la Mataifa ya Afrika
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 1980, uwanja huo ulitumika kuliandaa mechi kadhaa wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980 na Kombe la Mataifa ya Afrika, pamoja na nusu fainali kati ya Timu ya kitaifa ya Algeria na Timu ya kitaifa ya Misri.
Mashindano ya Vijana ya Dunia ya FIFA
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 1999, Uwanja wa Uhuru ulichaguliwa pamoja na viwanja vingine nane nchini Nigeria kuandaa Mashindano ya Dunia ya Vijana ya FIFA ya mwaka 1999.
Uwanja huo ulitumika kuaandaa mechi zote za Kundi C, moja ya mechi za Raundi ya 16, na moja ya mechi za robo fainali.
Kubadilisha jina
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Novemba 12, mwaka 2010, uwanja huo ulibadilishwa jina na kuwa Uwanja wa Obafemi Awolowo mpaka sasa .[2] Kubadilisha jina la uwanja huo kulitangazwa na rais wa wakati huo wa Nigeria, Dk Goodluck Jonathan, wakati alipomtembelea mjane wa Chifu Obafemi Awolowo, Chifu Bi. Hannah Idowu Dideolu Awolowo. [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.flickr.com/photos/jujufilm/5885877459/in/photolist-9Y7EiR-9YatA9-9YaXFd-9Y81ic-9YaPjW-9YaXa3-9Y7Xxp-9YaLo5-9YaMJo-9YaYVG-9Y8276-9YaM6j-9Y82S6-9YaNy7-9YaQfU-9YaZxW-9YaR6E-9YavZE-9Y7PLH-9YaFnA-9YaDpd-9Y7DCk-9Y7ChT-9Yauey-9YaEgY-9YaAbu-9YaGkQ-9Y7GcM-9Y7AAg-9Y7CXB-9YaBzU
- ↑ Awolowo Stadium At last Ilihifadhiwa 27 Desemba 2010 kwenye Wayback Machine. Nigerian Tribune, November 23, 2010.
- ↑ "Jonathan Renames Liberty Stadium in Ibadan after Awolowo", 14 November 2010. Retrieved on 2021-06-07. Archived from the original on 2011-01-07.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- World Stadiums: Liberty Stadium (Ibadan) Ilihifadhiwa 7 Juni 2021 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Obafemi Awolowo kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |