Uwanja wa Nyayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Uwanja wa kitaifa wa Nyayo ni uwanja wa azma tofauti tofauti mjini Nairobi, Kenya. Iko karibu na kituo cha mji. Uwanja huu unaweza kushikilia watu elfu thelathini na ulijengwa mwaka wa 1983. Hivi sasa hutumiwa zaidi kwa mechi ya kandanda. Klabu maarufu ya AFC Leopards huchezea mechi zao mengi za kinyumbani huko. Uwanja huu pia hutumika kwa Riadha na sherehe mbalimbali. Vifaa vingine katika uwanja wa nyayo ni pamoja na Gym na mita hamsini ya pahali pa kuogelea. Kukamilika kwa uwanja wa nyayo ulipatia Kenya nafasi ya kuwekwa katika jamii ya Mataifa yalioalikwa kushindania kuandaa michezo ya nne ya Pan African games mwaka wa 1987. Kenya ilinyakua nafasi hii na kuipa sifa kimataifa. Hivi uwanja wa kitaifa wa nyayo ulisababisha kujengwa kwa uwanja wa kimataifa wa Moi. Uwanja wa nyayo ulibadilishwa jina na kuwa uwanja wa kitaifa wa coca cola, baada ya kampuni hii ya kimataifa kushinda haki za kuipa jina mwezi wa februari 2009. Mpango huo alikuwa wa thamani ya dola milioni 1.5, na kampuni hii ya coca cola ingeweza kuipa jina, na kuirekebisha kwa miaka mitatu. Miezi mitatu tu baadaye, Coca Cola ilijiondoa kutoka kwenye mkataba, kwa sababu serikali ya Kenya ilitaka jina ya uwanja uwe uwanja wa kimataifa wa nyayo coca cola. [1] Makao makuu ya Shirikisho la Soka Kenya na Athletics Kenya, iko uwanja mkuu wa Nyayo. Yafuatayo ni orodha kina ya miundombinu katika uwanja;


a) Uwanja Mkuu.[hariri | hariri chanzo]

Miundo mikuu

 • Inakalisha watu 30,000.
 • Uwanja wa kandanda ni wa kiwango iliyokubaliwa na FIFA
 • Sherehe kama vile siku ya likizo ya kitaifa, mikutano, na hafla za kidini hufanyiwa huko.
 • Vyumba viwili vya kifahari vya mapumziko, na ofisi.
 • kituo cha vyombo vya habari kilicho na mtandao.
 • Floodlights.

b) Aquatic Centre.[hariri | hariri chanzo]

Miundo mikuu.

 • Spectator terraces kwa 2000 pax.
 • A filtration kupanda.
 • 50 x 25 m Pool.
 • wazi kwa umma wiki yote.
 • Lifeguards ambao wamefunzwa.

c) Indoor Gymnasium.[hariri | hariri chanzo]

Miundo mikuu

 • Inaweza kushikilia watu 2500.
 • Uwanja kuu iliyo ndani ya jengo - Ndipo ligi ya kitaifa ya mpira wa kikapu inpoendeleza hafla zake.
 • Chumba cha kukulia.
 • Uwanja ulioko ndani na ambayo imefunikwa.
 • Mpira wa kikapu, dondi, Badminton, Martial arts na ustawi wa utendaji.
 • Mbinu za kisasa za kuhesabu alama.

d) Eneo ya mafunzo ya Voliboli na mpira wa mikono.[hariri | hariri chanzo]

Miundo mikuu

 • Terraces inayowezo wa kushikilia watu 1500
 • Matukio ya kijamii yanaweza aandaliwa huko.

References[hariri | hariri chanzo]

 1. Nyayo Stadium no longer on the Coke side of life. Daily Nation. Iliwekwa mnamo 2009-05-26.

Viunganish vya nje[hariri | hariri chanzo]


Majiranukta kwenye ramani: 1°18′15.1″S 36°49′28.1″E / 1.304194°S 36.824472°E / -1.304194; 36.824472