Utata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya utata: ni sungura au bata?

Utata ni hali ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Utata hutokea pale mtu wa upande wa kikomo anaposhindwa kupata maana iliyokusudiwa na chanzo.

Mambo yanayosababisha utata ni kama: 1. Matumizi yasiyo sahihi ya alama za uandishi 2. Kutokuzingatia muktadha katika matumizi ya lugha 3. Kutumia maneno yenye picha, kwa mfano taswira au jazanda 4. Tungo moja kuwa na maana zaidi ya moja; mfano neno kata.

Utata hujitokeza katika mazingira tofautitofauti.

Aina ya kwanza ni utata wa neno au maneno. Baadhi ya maneno katika lugha ya Kiswahili na nyinginezo yana maana zaidi ya moja; kwa mfano barabara inaweza kumaanisha "njia pana" au "sawasawa".

Aina ya pili ni utata wa sentensi; sentensi tata ni ile yenye maana zaidi ya moja na mara nyingi maana zenyewe haziko wazi kabisa. Sentensi moja inawezekana kueleweka hivi au vile na bado maana zote zikawa sahihi. Sababu ni: kutumia misimu, uwezo wa neno moja kuwa na maana zaidi, kutozingatia taratibu za uandishi, kutumia maneno bila kuzingatia mazingira au muktadha unaohusika, kuwepo kwa mofimu ya hali ya kutenda.

Jinsi ya kuondoa utata[hariri | hariri chanzo]

Katika lugha kuwe na mkazo tofauti ili kutofautisha maana, kuzingatia matumizi sahihi ya alama za uandishi, kutumia maneno kwa muktadha maalumu, kutofautisha matumizi ya maneno yenye mzizi -amba-.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utata kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.