Ujanseni
Ujanseni ulikuwa tapo la teolojia ya Kanisa Katoliki (hasa nchini Ufaransa) katika karne ya 17 na ya 18. Tapo hilo lilisisitiza dhambi ya asili, uovu wa binadamu uliosababishwa nayo, haja ya neema ya Mungu na uteule kwa kudai linafuata mafundisho ya Augustino wa Hippo.
Tapo lilitokana na vitabu vya mwanateolojia wa Uholanzi Cornelius Jansen vilivyochapishwa baada ya kifo chake (1638). Rafiki yake, abati Jean Duvergier de Hauranne, alisambaza mafundisho yake kwanza, na alipokufa yeye pia (1643) juhudi ziliendelezwa na Antoine Arnauld, lakini pia na Pierre Nicole, Blaise Pascal na Jean Racine.
Ujanseni ulipingwa na wengi, hasa Wajesuiti, kwa kuona unafanana na Ukalvini.[1]
Mwaka 1653, kwa hati Cum occasione, Papa Innocent X alilaani kama uzushi kauli tano za Wajanseni.[1] Viongozi wao walijaribu kulegeza msimamo wao bila kuachana nao kabisa, lakini hatimaye walihukumiwa tena na hati Unigenitus Dei Filius ya Papa Klementi XI mwaka 1713.[2]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Carraud, Vincent (2008-01-21) [Created 2007-06-20]. "Le jansénisme". Bibliothèque électronique de Port-Royal (lecture) (kwa French). Société des Amis de Port-Royal. ISSN 1776-0755. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-11.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Toon Quaghebeur, "The Reception of Unigenitus in the Faculty of Theology at Louvain, 1713-1719", Catholic Historical Review 93/2 (2007), pp. 265-299.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Abercrombie, Nigel (1936). The origins of Jansenism. Oxford studies in modern languages and literature. Oxford: Clarendon Press. OCLC 599986225.
- Hamscher, Albert N. (1977). "The Parlement of Paris and the social interpretation of early French Jansenism". Catholic Historical Review. 63 (3). Catholic University of America Press: 392–410. ISSN 0008-8080. JSTOR 25020157.
- Doyle, William (1999). Jansenism: Catholic resistance to authority from the Reformation to the French Revolution. Studies in European history. New York: St. Martin's Press. ISBN 9780312226763.
- Hudson, David (1984). "The 'Nouvelles Ecclésiastiques', Jansenism, and Conciliarism, 1717-1735". Catholic Historical Review. 70 (3). Catholic University of America Press: 389–406. ISSN 0008-8080. JSTOR 25021866.
- Ogg, David. Europe in the 17th Century (6th ed. 1952) pp 323-64.
- Schmaltz, Tad M. (Jan 1999). "What has Cartesianism to do with Jansenism?". Journal of the History of Ideas. 60 (1). University of Pennsylvania Press: 37–56. doi:10.1353/jhi.1999.0009. ISSN 0022-5037. JSTOR 3653999.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Van Kley, Dale (Fall 2006). "The rejuvenation and rejection of Jansenism in history and historiography: recent literature on eighteenth-century Jansenism in French". French Historical Studies. 29 (4). Duke University Press: 649–684. doi:10.1215/00161071-2006-016. ISSN 0016-1071.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Strayer, E. Brain, Suffering Saints: Jensenits and Convulsionaries in France, 1640–1799 (Eastborne, Sussex Academic Press, 2008)
- Crichton. D. J., Saints or Sinners?: Jansenism and Jansenisers in Seventeenth Century France (Dublin, Veritas Publications, 1996)
- Swann Julian, Politics and the Parliament of Paris under Louis XV 1754–1774, (Cambridge, Cambridge University Press, 1995)
- Doyle William, Jansenism: Catholic Resistance to Authority from the Reformation to the French Revolution: Studies in European History (Basingstoke, Macmillan Press Ltd, 2000)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Provincial Letters by Blaise Pascal Archived 24 Agosti 2017 at the Wayback Machine. (1656)
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ujanseni kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |