Ufundi wa vita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nakala ya Ufundi wa Vita iliyoandikwa kwenye kanda za bamboo

Ufundi wa vita (kwa Kichina 孫子兵法 pinyin Sūnzǐ bīngfǎ Sunzi kuhusu ufundi wa vita) ni kitabu cha mwandishi Mchina Sunzi kuhusu mikakati ya vita. Hutazamwa kama kitabu cha kwanza kinachojulikana katika fani hii kikisomwa hadi leo hii na wanafunzi na viongozi wa siasa, uchumi na jeshi.

Kitabu kinaeleza umuhimu wa kutumia vifaa vyote vinavyopatikana kwa kufikia shabaha na umuhimu wa kuvitumia kulingana na hali halisi na kuwa tayari ya kubadilisha mbinu mara kwa mara.

Viongozi kama Mao Zedong (China), jenerali Vo Nguyen Giap (Vietnam), jenerali Douglas MacArthur (Marekani) na wengine walikisoma na kujifunza kutoka kitabu cha Sunzi.

Muundo wa kitabu[hariri | hariri chanzo]

Kitabu kina milango 13 inayojadili pande mbalimbali za kuandaa vita na kuviendesha.

 1. Mkakati au namna ya kupanga vita
 2. Namna za kuendesha vita
 3. Mikakati ya mashambulizi
 4. Mbinu za kutumia rasilimali za kijeshi
 5. Namna ya kutumia nguvu
 6. Udhaifu na nguvu
 7. Namna za kuongoza jeshi
 8. Njia tisa za kutumia rasilmali za kijeshi
 9. Jeshi katika mwendo
 10. Eneo la vita
 11. Aina tisa za maeneo
 12. Kutumia moto katika mashambulio
 13. Matumizi ya wapelelezi

Mafundisho[hariri | hariri chanzo]

Sunzi anaonya ni heri kuepukana na vita kwa sababu vinaharibu dola na taifa. Jambo muhimu ni kwanza kubatilisha mkakati wa adui, pili kuvunja ushirikiano wa adui na wenzake, tatu kupiga vita na kushinda kama hatua za kwanza na za pili zimeshindikana.

Sunzi anajadili hatari ya vita virefu anayotaja kama tishio hasa kwa kutunza jeshi lake na uwezo wake. Kutokana na hatari hii ni shabaha muhimu kuepukana na mapigano marefu.

Anataka kiongozi awe na utulivu wa kusubiri lakini kutumia nguvu yote kama ni lazima kuingia katika mapigano. „Mpiganaji mwenye hekima atatafuta nafasi inayozuia kushindwa kwake na hasiti kutumia muda sahihi wa kumshinda adui haraka iwezekanavyo."

Sunzi aliandika: „Ufundi mkuu vitani ni kuvunja upinzani wa adui bila mapigano"

Matoleo[hariri | hariri chanzo]

[Toleo la Kiingereza lilitafsiriwa 1994 na Ralph D. Sawyer, limechapishwa mwaka 2003