Nenda kwa yaliyomo

Kanghagha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Turdoides)
Kanghagha
Zogoyogo wa Sharpe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia: Leiothrichidae (Ndege walio na mnasaba na kanghagha)
Swainson, 1832
Ngazi za chini

Jenasi 13:

Kanghagha au zogoyogo ni ndege wa familia Leiotrichidae. Wanafanana na mikesha wa familia Turdidae. Wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika na Asia. Spishi za Afrika zina rangi za kahawa, nyeusi, kijivu na nyeupe, lakini spishi nyingi za Asia zina rangi kali pia kama nyekundu na njano. Takriban spishi zote huenda kwa makundi wakiwasiliana kwa sauti. Mara kwa mara hupiga kelele sana, kwa sababu yake huitwa mpayupayu pia (“babbler” au “chatterer” kwa Kiingereza). Hula wadudu hasa lakini beri pia; spishi kubwa hula mijusi na panya wadogo na spishi kadhaa hula beri tu. Hulijenga tago lao kwa vitawi na kulificha katika vichaka vizitu. Jike huyataga mayai 2-5. Spishi kadhaa hujenga tago kwa kundi; jike mmoja tu hutaga mayai na ndege wengine husaidia kuwalinda makinda na kuwaletea chakula.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia

[hariri | hariri chanzo]