Nenda kwa yaliyomo

Trilojia ya filamu za Sabata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfululizo wa Filamu za Sabata
Kasha ya DVD ya mfululizo wa filamu za Sabata.
Kasha ya DVD ya mfululizo wa filamu za Sabata.
Imeongozwa na Gianfranco Parolini
Imetungwa na Renato Izzo
Gianfranco Parolini
Imetaarishwa na Alberto Grimaldi
Nyota Lee Van Cleef
Yul Brynner
Muziki na Marcello Giombini
Bruno Nicolai
Imesambazwa na MGM/UA
Muda wake Dk. 315
Imetolewa tar. 1969-1971
Nchi Italia
Lugha Kitaliano

Trilojia ya Sabata ni jina la kutaja aina ya mifululizo ya filamu za Spaghetti Western zilizotolewa mnamo mwaka wa 1969 na 1971. Filamu zilioongozwa na Bw. Gianfranco Parolini na kuchezwa na nyota Lee van Cleef katika sehemu ya kwanza ya Sabata, Yul Brynner katika sehemu ya pili ya Sabata - Adiós, Sabata, na kisha Lee Van Cleef akarudia tena katika mfululizo wa tatu uliojulikana kwa jina la Return of Sabata.

Mfululizo wa hadithi

[hariri | hariri chanzo]

Katika Sabata

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu ya: Sabata

Lee Van Cleef amecheza akiwa kama mtu aliye kimya saa zote, mpambanaji pekee aliyepewa mpango na viongozi wadogo wa mji wa Texas kwenda kuwaibia benki yao wenyewe na kwenda kuiuza mjini kunako karibu na njia ya reli. William Berger aliyecheza kama Banjo, alilipinga swala hilo.

Katika Adiós, Sabata

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu ya: Adiós, Sabata

Katika filamu hii Yul Brynner amechukua nafasi kutoka kwa mwigizaji wa awali bwana Lee Van Cleef, ambaye alicheza katika Sabata ya kwanza na ya tatu.

Hapo awali filamu ilibidi iyende kwa jina la Indio Black, lakini jina lilibadilishwa kutokana kwamba filamu ya kwanza ilifanya vizuri kwa jina la Sabata na ikaonekana kuwa na wapenzi wengi kuliko. Filamu hii ilibdi acheze Lee Van Cleef, lakini Cleef hakucheza kwasababu alikuwa anacheza filamu ya The Magnificent Seven Ride, humo alitumia jina lile lile la Chris Adams, ambalo Brynner alibebea umaarufu katika filamu ya awali ya The Magnificent Seven.

Ilikuwa ndani ya nchi Mexiko iliyokuwa chini Dola la Maximilian I, Sabata alikodiwa na kiongozi wa guerilla bwana Señor Ocaño kwenda kuiba wagonload (Farasi mwenye kijumba nyuma) wa dhahabu kutoka mikononi mwa majeshi ya Kiaustrian. Sabata na rafiki zake wawili Escudo na Ballantine walifanikiwa kulitwaa wagon, lakini hawakukuta dhahabu bali waliukuta mchanga katika wagon hiyo, na dhabu ilikuwa ishachukuliwa na Amiri jeshi mkuu wa Kiaustria bwana Skimmel. Kwa hiyo Sabata akapanga mpango wa kurudisha dhahabu hizo.

Katika Return of Sabata

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu ya: Return of Sabata

Lee Van Cleef amerudi tena kwa jina la Sabata, ambaye anaelekea zake katika mji mdogo wa Texas kwa lengo la kulipiza kisasi kwa wale wezi waiomgeuka, huku akiwa na wazo la kutaka kuziiba tena zile hela walizomwibia yeye hapo awali.

Matoleo ya Sabata katika DVD

[hariri | hariri chanzo]

The Sabata Trilogy ilitolewa katika DVD na MGM/UA mnamo mwezi wa Oktoba katika mwaka wa 2005.

Filamu nyingine za Sabata

[hariri | hariri chanzo]

Kama ilivyozoeleka mafanikio ya filamu za Spaghetti Western, kama vile Dollars Trilogy au Django, matoleo mengine mengi ya kuiigizia Sabata yalitolewa. Sabata hizo inaiihusiha Wanted Sabata, iliyongozwa na Bw. Roberto Mauri na kuchezwa na nyota Brad Harris, vilevile Arriva Sabata!, iliyoongozwa na Bw. Tulio Demicheli na kuchezwa na nyota Peter Lee Lawrence, ambayo ilitengenezwa mnamo mwaka wa 1970.

Watch Out Gringo! Sabata Will Return, ilitengenezwa mnamo mwaka wa 1972, na iliongozwa na Bw. Alfonso Balcázar na Pedro Luis Ramírez na kuchezwa na nyota George Martin. Hamna hata moja katika hizi zilizojumlisha katika mfululizo wa Sabata asilia.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]