Sabata
Sabata | |
---|---|
| |
Imeongozwa na | Gianfranco Parolini |
Imetungwa na | Renato Izzo Gianfranco Parolini |
Imetaarishwa na | Alberto Grimaldi |
Nyota | Lee Van Cleef William Berger |
Muziki na | Marcello Giombini |
Imehaririwa na | Edmond Lozzi |
Imesambazwa na | MGM/UA |
Muda wake | Dk. 111 |
Imetolewa tar. | 2 Septemba 1970 |
Nchi | Italia |
Lugha | Kitaliano |
Sabata (kwa Kitaliano: Ehi amico ... c'è Sabata, hai chiuso!, kwa haraka-haraka inatafsrika kama "Hoya washkaji... huyo ni Sabata, mmekwisha!"), ni filamu ya Spaghetti Western iliyotolewa mnamo 1969. Filamu iliongozwa na Gianfranco Parolini. Ni toleo la kwanza la Mfululizo wa Filamu za Sabata ziilizotengenezwa na Bw. Parolini, na kuchezwa na nyota Lee Van Cleef akiwa kama jina la picha. Kibwagizo cha filamu kinatoka wimbo wa mwaka 1957 ulioimbwa na Bw. Frankie Laine.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Muhtasari wa filamu
[hariri | hariri chanzo]Sabata, ni mtu asiyeoongea sana akiwa na silaha mkononi, amewasili katika mji mdogo wa Texas kwenda kuzuiya wizi wa benki, na kugundua kuwa mpango huo umepangwa na vigogo wa mjini hapo, ambao walitaka kuuza mji huo kwa ajili ya njia ya reli.
Sabata akamteka kiongozi wao, Stengel, ambaye baadaye alituma wahuni kadhaa kwenda kumwangamiza Sabata, mmoja kati ya wauaji hao alikuwemo Banjo, aliitwa hivyo kwakuwa alikuwa kibeba kigizo chenye ala za muziki ambacho kilikuwa kimeficha bunduki ndani yake.
Washiriki
[hariri | hariri chanzo]- Lee Van Cleef amecheza kama Sabata
- William Berger amecheza kama Banjo
- Ignazio Spalla amecheza kama Carrincha
- Aldo Canti amecheza kama Indio
- Franco Ressel amecheza kama Stengel
- Antonio Gradoli amecheza kama Ferguson
- Linda Veras amecheza kama Jane
- Claudio Undari amecheza kama Oswald
- Gianni Rizzo amecheza kama Judge O'Hara
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ehi amico... c'è Sabata, hai chiuso! at the Internet Movie Database
- (Kiingereza) Sabata katika Allmovie
- Sabata at Shobary's Spaghetti Westerns Archived 17 Septemba 2008 at the Wayback Machine.