Trikomonasi
Mandhari
Trikomonasi ni mojawapo kati ya maradhi ya zinaa na husababishwa na maambukizi ya protozoa anayefahamika kwa jina la kisayansi Trichomonas vaginalis.
Dalili
[hariri | hariri chanzo]Ugonjwa huo husababisha mwasho na karaha katika uke (kwa wanawake) na katika mfereji wa mkojo (kwa wanaume). Hayo yanaweza yakatokea siku 5-28 baada ya kupatwa, lakini wanawake 70% na wanaume 50% hawaoni dalili wanapopatwa. Ingawa ni hivyo, wanaweza kueneza ugonjwa wakifanya mapenzi kwa njia yoyote.
Kinaganaga zaidi:
- Kwa wanawake: kuwashwa moto ukeni wakati wa kukojoa, kutokwa na uchafu wenye harufu kama ya samaki, kuwashwa sehemu za uke, kuvimba kwa mashavu ya via vya uzazi, njia ya uke kuonekana nyekundu na kuvimba, hatimaye maumivu makali wakati wa kukojoa na wa kujamiiana.
- Kwa wanaume: kutoka uchafu kwenye uume, kuwashwa sehemu za uume, kuchubuka sehemu za siri, hatimaye maumivu makali wakati wa kukojoa na wa kujamiiana.
Uenezi
[hariri | hariri chanzo]Imekadiriwa kuwa Wamarekani milioni tano huambukizwa trikomonasi kila mwaka. Kimataifa mwaka 2015 waliopatwa na ugonjwa huo walikuwa 122 milioni, wanawake wakiwa wengi kuliko wanaume.
Tiba
[hariri | hariri chanzo]Trikomonasi huweza kutibiwa kwa urahisi na antibiotiki.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Trichomoniasis at Centers for Disease Control and Prevention
- Vaginitis/Vaginal infection fact sheet from the National Institute of Allergies and Infections. The first version of this article was taken from this public domain resource.
- eMedicine Health Trichomoniasis Archived 2008-05-22 at the Wayback Machine
| Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Trikomonasi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |