Timo Werner
Timo Werner (alizaliwa 6 Machi 1996) ni mchezaji wa soka wa Ujerumani ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig na timu ya taifa ya Ujerumani.
Timu alizochezea
[hariri | hariri chanzo]VfB Stuttgart
[hariri | hariri chanzo]Werner aliwakilisha klabu hiyo katika ngazi mbali mbali za vijana. Katika msimu wa 2012-13, alipandishwa katika upande wa U-19 yaaani chini ya miaka 19 licha ya kuwa alikuwa na umri wa miaka kumi na sita wakati huo. Alifunga magoli 24 wakati alishinda medali ya Dhahabu ya U-17 Fritz Walter mnamo mwaka 2013.[1]
RB Leipzig
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 11 Juni 2016, Werner alikubali mkataba wa miaka minne katika klabu ya RB Leipzig kwa ada ya kuripotiwa ya uhamisho wa milioni 10 na ulikuwa ndo uhamisho mkubwa wa klabu hiyo katika historia.
Mnamo 26 Septemba, 2016, alikua mchezaji wa kwanza kucheza kwenye mechi 100 za Bundesliga wakati akiwa katika mechi ambayo alicheza dhidi ya FC Köln akiwa na miaka 20 na siku 203 Kwa kufanya hivyo alitoa rekodi ya hapo awali iliyoshikiliwa na Julian Draxler kwa siku 22, ingawa alizidiwa tena na Havertz mnamo 2019.
Werner alimaliza msimu wa Bundesliga wa mwaka 2016- 17 akiwa na magoli 21, na kumfanya kuwa mfungaji bora wa mabao wa Ujerumani na kuisaidia klabu ya RB Leipzig kufuzu katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo.
Kazi ya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Werner aliiwakilisha Ujerumani katika kiwango cha vijana, akicheza kwa timu za chini ya miaka 15, 16, 17, 19 na 21, alifunga magoli 34 katika mechi 48 kwa jumla.
Mnamo 2010, alifunga hat-trick yaani magoli matatu kwenye mechi yake ya kwanza ya Ujerumani chini ya miaka 15 kwenye mechi dhidi ya Poland. Miaka miwili baadaye, alikuwa sehemu ya timu ya taifa ya Ujerumani iliyomaliza kwa kufanya vizuri katika Mashindano ya Ulaya ya chini ya miaka 17.
Werner aliitwa kwenye kikosi kikuu cha Ujerumani mnamo mwaka 2017 na kocha mkuu Joachim Löw akiwa na miaka 21 kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Uingereza na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2018 dhidi ya Azerbaijan mnamo tarehe 26 Machi 2017.[2]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Timo Werner kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |