Tiberia
Mandhari
(Elekezwa kutoka Tiberias)
Tiberia (pia: Tiberias; awali: Yam Ha-Kineret) ni mji wa Israeli kwenye pwani ya ziwa Galilaya, ambalo pengine linaitwa ziwa au bahari ya Tiberia (Yoh 6:1).
Mji huo ni maarufu kwa sababu Injili zinautaja kuhusiana na Yesu kuzidisha mikate na samaki kwa ajili ya umati (Yoh 6:23) na baada ya ufufuko wake kuwaandalia wanafunzi wake mikate na samaki juu ya makaa (Yoh 21:1).
Mwaka 2019 idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa 44,779 [1].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Population in the Localities 2019" (XLS). Israel Central Bureau of Statistics. Retrieved 16 August 2020.
Makala kuhusu Israeli bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |