Nenda kwa yaliyomo

Nge-mjeledi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Thelyphonida)
Nge-mjeledi
Nge-mjeledi (Mastigoproctus giganteus) akionyesha pedipalpi na mjeledi
Nge-mjeledi (Mastigoproctus giganteus) akionyesha pedipalpi na mjeledi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Oda: Thelyphonida
Ngazi za chini

Familia 1 na nusufamilia 4:

Nge-mjeledi (kutoka Kiingereza whip scorpion) ni arithropodi wa oda Thelyphonida katika ngeli Arachnida wafananao na nge wa kawaida. Kama hawa wana miguu minane na pedipalpi zenye gando. Mjeledi wa jina lao ni aina ya mkia mrefu na mwembamba. Kama kawaida mwili wao una sehemu mbili: kefalotoraksi (cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio zilizoungwa kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija. Nge-mjeledi wana macho manane, mawili mbele ya kefalotoraksi na matatu kwa kila upande wa kichwa. Pedipalpi zao zinafanana na zile za nge, lakini zina mwiba nyuma ya gando na maneno magumu kwa kitako chao ambayo hutumika kwa kukamua mawindo. Miguu sita tu hutumika kwa kutembea. Jozi ya kwanza imekuwa mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio.

Nge-mjeledi hawana sumu lakini wana matezi yanayotoa mchanganyiko wa asidi ya asetiki na asidi ya kapriliki wakisumbuliwa. Hula arithropodi wengine, pengine nyungunyungu na makonokono uchi pia.

Katika Afrika kuna spishi moja tu, Etienneus africanus, inayotokea Afrika ya Magharibi.

Makala hii kuhusu "Nge-mjeledi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili whip scorpion kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni nge-mjeledi.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.