Nenda kwa yaliyomo

Chati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Thamnolaea)
Chati ya wawakilishi wa Bunge la 38 la Kanada.

Chati (kutoka ing. chart[1]) za data au jedwali, ambapo taarifa inawakilishwa na michoro ya aina mbalimbali. Chati inaweza kuwakilisha takwimu za data za simu, kazi au aina fulani za muundo wa ubora na hutoa maelezo tofauti.

Neno chati kama uwakilishi wa takwimu ya data ina maana nyingi:

Chati ya data ni aina ya mchoro au grafu, ambayo hupanga na inawakilisha tarakimu.

Ramani ambazo huwa na maelezo ya ziada kwa madhumuni maalum mara nyingi hujulikana pia kama chati, kama ramani za mabaharia na wanaanga.

Wakati mwingine michoro ya kodi za msingi za muziki huitwa chati au chati ya rekodi maarufu za muziki.

Kawaida chati hutumika kurahisisha uelewaji wa data kubwa na uhusiano kati ya sehemu za data hizo. Kawaida zinaweza kusomwa kwa haraka zaidi. Zinatumika katika nyanja mbalimbali kama vile sayansi na hesabu [2], biashara [3], n.k. na zinaweza kuchorwa kwa mkono (mara nyingi kwenye karatasi ya grafu) au kwa kompyuta kwa kutumia programu maalumu ya chati.

Aina fulani za chati ni bora zaidi kwa kuwasilisha data kuliko nyingine. Kwa mfano, data inayowakilisha namba zinazobadilika kwa kipindi cha muda (kama vile "mapato ya kila mwaka kutoka 1990 hadi 2000") zinaweza kuonyeshwa kwa ubora zaidi kwa kutumia chati ya mstari.

Aina za chati

[hariri | hariri chanzo]

Chati nne zinazotumika kwa wingi

[hariri | hariri chanzo]

Chati zisizotumika kwa wingi

[hariri | hariri chanzo]

Chati maarufu zilizopewa majina

[hariri | hariri chanzo]
  1. kiasili kutoka gir. χάρτης khhartis yaani karatasi
  2. Graphs in Science and Mathematics on JSTOR
  3. "Typology of business charts". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-06. Iliwekwa mnamo 2018-10-05.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.