Gesi ya machozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tear gas)
Gesi ya machozi ikitumika nchini Ufaransa mnamo 2007
Mlipuko wa gesi ya machozi ulilipuka juu ya kuruka huko Ugiriki

Gesi ya machozi ni silaha ya kikemia inayosababisha maumivu kwenye macho na pia kwenye njia ya pumzi. Inatumiwa kama silaha isiyoua lakini kwa viwango vikubwa inaweza kuleta madhara makubwa zaidi, hadi kusababisha kifo.

Kwenye jicho inakera neva za tezi za machozi zinazoanza kutoa machozi.

Kuna dawa mbalimbali zinazotumika kwa kutengeneza gesi ya machozi,

Gesi hiyo hutumiwa kwa kawaida na polisi kwa kutawanya umati mkubwa wa watu, kuvunja maandamano au kutuliza ghasia[1].

Hairuhusiwi kuitumia vitani maana matumizi ya gesi dhidi ya wanajeshi hukataliwa na mikataba ya kimataifa, baada ya vita ya gesi sumu wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Hatua za kujikinga[hariri | hariri chanzo]

Njia bora zaidi ya kujikinga ni kuvaa kichuja hewa usoni. Pale ambapo hakipatikani, miwani ya kuogelea (goggles) inafaa kukinga macho, pamoja na kitambaa kinyevu kinachoshikwa mbele ya mdomo na pua kama kinga ya njia za pumzi. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Tear gas—harassing agent or toxic chemical weapon?". JAMA 262 (5): 660–3. August 1989. PMID 2501523. doi:10.1001/jama.1989.03430050076030. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 October 2013.  Unknown parameter |vauthors= ignored (help); Check date values in: |date=, |archivedate= (help)
  2. "Gezi park protesters bring handmade masks to counter police tear-gas rampage". Hürriyet Daily News. 
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gesi ya machozi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.