Tambarare ya China Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tambarare ya China Kaskazini na Mto Njano (unaoitwa humu jina la Kihispania "Rio Amarillo").

Tambarare ya China Kaskazini (kwa Kichina: 華北平原; pinyin: Huáběi Píngyuán) ni tambarare kubwa nchini China. Inaenea katika kaskazini ya China pande zote mbili za Mto Njano.

Asili ya tambarare hii ni bonde kubwa lililojazwa polepole na mashapo ya Mto Njano katika kipindi cha miaka milioni kadhaa. Matope yaliyoletwa na Mto Njano yaliunda ardhi yenye rutuba na hivyo tambarare ilikuwa eneo la kilimo tangu kale. Mafuriko ya mara kwa mara, lakini pia hatari ya ukame wakati wa kucheza kwa mvua, yalisababisha ushirikiano wa watu kwa ajili ya kujenga mifereji na kupanga umwagiliaji. Hivyo tambarare hiyo imekuwa pia eneo ambako madola ya kwanza ya China yalianzishwa.

Eneo lote la tambarare ni takriban km² 409,500 na sehemu kubwa iko mita 50 juu ya usawa wa bahari. Katika eneo hili kubwa pasipo vizuizi vya milima, lugha na utamaduni wa pamoja viliweza kukua.

Flag-map of the People's Republic of China.svg Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tambarare ya China Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.