Tai Mlanyoka
Tai mlanyoka | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Tai walanyoka ni ndege mbua wakubwa kiasi wa nususfamilia Circaetinae katika familia Accipitridae. Tai wa Ufilipino ni labda mwana wa nusufamilia hii, kwa sababu chunguzi za ADN zimeonyesha mnasaba wake. Ndege hawa wana makucha marefu ili kukamata uwimbo na domo kubwa lenye ncha kwa kulabu ili kupapura nyama. Uwezo wao wa kuona kwa macho ni mzuri kabisa na hutambua uwimbo kwa mbali sana. Tai walanyoka hula nyoka hasa (isipokuwa tai pungu) lakini mijusi na mamalia wadogo pia na pengine ndege na wadudu wakubwa. Hujenga tago lao mtini ambola limefichwa vizuri kati ya majani. Jike hulitaga yai moja tu, au pengine mayai mawili.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Circaetus beaudouini, Tai wa Beaudouin (Beaudouin’s Snake Eagle)
- Circaetus cinerascens, Tai Miraba Magharibi (Western Banded Snake Eagle)
- Circaetus cinereus, Tai Mlanyoka Kahawia (Brown Snake Eagle)
- Circaetus fasciolatus, Tai Miraba Kusi (Southern Banded Snake Eagle)
- Circaetus gallicus, Tai Madole-mafupi (Short-toed Snake Eagle)
- Circaetus pectoralis, Tai Kidari-cheusi (Black-chested Snake Eagle)
- Dryotriorchis spectabilis, Tai Mlanyoka wa Kongo (Congo Serpent Eagle)
- Eutriorchis astur, Tai Mlanyoka wa Madagaska (Madagascar Serpent Eagle)
- Terathopius ecaudatus, Tai Pungu (Bateleur (Eagle))
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Pithecophaga jefferyi (Philippine Eagle) - cheo sina hakika
- Spilornis cheela (Crested Serpent Eagle)
- Spilornis elgini (Andaman Serpent Eagle)
- Spilornis holospilus (Philippine Serpent Eagle)
- Spilornis kinabaluensis (Mountain Serpent Eagle)
- Spilornis klossi (Great Nicobar Serpent Eagle)
- Spilornis minimus (Central Nicobar Serpent Eagle)
- Spilornis rufipectus (Sulawesi Serpent Eagle)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Tai wa Beaudouin
-
Tai madole-mafupi
-
Tai kidari-cheusi
-
Tai mlanyoka wa Kongo
-
Tai mlanyoka wa Madagaska
-
Pungu
-
Philippine eagle
-
Crested serpent eagle
-
Andaman serpent eagle
-
Philippine serpent eagle