Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Tanzania
Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (kifupi: TAKUKURU) ni taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kupambana na rushwa. Ni idara inayojitegemea ambayo ipo chini ya Ofisi ya Rais.
Makao makuu yapo eneo la Chamwino, Dodoma.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Hapo awali, taasisi hiyo ilikuwa ikijulikana kama Taasisi ya kuzuia Rushwa ya Tanzania (TAKURU). Taasisi ya Kuzuia Rushwa iliundwa na Sheria namba 2 ya mwaka 1974 ambayo ilipitisha kuundwa kwa Kikosi cha Kuzuia Rushwa, baada ya kuifanyia marekebisho Sheria ya Kuzuia Rushwa Namba 16 ya mwaka 1971. Kikosi cha Kuzuia Rushwa kilianzishwa rasmi tarehe 15 Januari 1975 kwa tamko la Serikali Namba 17 la 1975[1].
Kabla ya mwaka wa 1975 shughuli za kuzuia rushwa zilifanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo jeshi la polisi lilipewa jukumu zima la kupambana na rushwa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-29. Iliwekwa mnamo 2021-04-29.