Susanne Wenger

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msitu mtakatifu wa Osun mjini Oshogbo inajaa sanaa iliyoumbwa na Susanne Wenger
Nyumba ya hekalu katika patakatifu pa Osun iliyotungwa na Wenger

Susanne Wenger, pia Adunni Olurisa, (* 4 Julai 1915 mjini Graz (Austria); † 12 Januari 2009 mjini Oshogbo, Nigeria) alikuwa msanii kutoka Austria aliyekaa muda mrefu Nigeria na kuunganisha mitindo ya sanaa za Ulaya na Afrika. Aliingia katika dini ya jadi ya Wayoruba akatambuliwa kama kuhani na kupewa jina la kineyeji.

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Susanne Wenger alizaliwa Austria kama mtoto wa wazazi Waaustria-Waswisi. Mjini Graz alianza kusoma sanaa akaendela kusoma uchoraji huko Vienna. Alishiriki katika mapambano ya kisiasa akapinga maungano ya Austriana Ujerumani. Wakati wa utawala wa kifashisti hakuonyesha picha zake. Baada ya vita alichora kwa ajili ya magazeti fulani yenye mwelekeo wa kijamii.

Alitembelea Italia, Uswisi na Ufaransa alipoolewa na Mjerumani Ulli Beier. Pamoja na Beier alihamia Nigeria ambako mumewe alipewa nafasi ya kufundisha kwenye chuo kikuu cha Ibadan.

Baada ya kufika Nigeria Wenger aligonjeka na kifua kikuu. Madaktari walishindwa kumsaidia hadi alitembelewa na babalawo au mganga wa Kiyoruba aliyeweza kumtibu. Baada ya uponyaji huu Wenger alijishughulisha sana na utamaduni, dini na sanaa ya Wayoruba akajenga nyumba yake mjini Oshogbo. Hapa alitumia muda mwingi katika msitu ulio patakatifu pa mungu-mama Osun. Ilipoonekana ya kwamba msitu huu ulikuwa hatarini kuharibiwa alinunua eneo na kupamba eneo la patakatifu kwa kazi za sanii zake.

Alifundisha wasanii wengi Wanigeria akishirikiana nao katika shule yake ya „New Sacred Art“. Mume wake alikaa naye lakini baadaye alirudi Ujerumani wakati Wenger alibaki Oshogbo. Baada ya kuingizwa katika siri za dini ya Kiyoruba akapewa cheo cha kuhani na jina la Adunni Olosuria. Msitu mtakatifu wa Osun ulipokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

  • Kunst als lebendiges Ritual, Iwalewa-Haus, Bayreuth 1991.
  • Mit Wolfgang Denk: Susanne Wenger - Tief in Dir bist Du oh Mensch der Gott als Baum, als Stein, als Tier: eine biographische Collage, Ausstellungskatalog Kunsthalle Krems, 1995, ISBN 3-901261-02-8.
  • Mit Gert Chesi: Ein Leben mit den Göttern, 1980, ISBN 3-85399-004-5

Tovuti[hariri | hariri chanzo]