Stratolaunch Roc

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Stratolaunch Roc
Ulinganifu wa Stratolaunch Roc na ndege kubwa zingine:      Stratolaunch Roc      Hughes H-4 Hercules      Antonov An-225      Airbus A380-800      Boeing 747-8

Stratolaunch Roc (ing. en:Scaled Composites Stratolaunch "Roc") ni eropleni kubwa zaidi duniani tangu kuruka mara ya kwanza katika mwezi wa Aprili 2019[1].

Mfumo[hariri | hariri chanzo]

Ndege hii imetengenezwa kwa kutumia ndege mbili za Boeing 747-400 ilhali injini, chumba cha rubani, magurudumu na haidroli za ndege hizi ilitumiwa. Ndege mpya ina upana mkubwa wa mabawa wa mita 117. Chini ya mabawa kuna sehemu mbili za pekee, na mzigo wa roketi utabebwa katikati chini ya mabawa[2].

Marubani hutumia chumba kwenye sehemu ya kulia, ilhali chumba cha rubani upande mwingine ni tupu.

Hata kama Stratolaunch Roc ni ndege kubwa duniani kufuatana na vipimo vyake, ndege ya Antonov An-225 kutoka Ukraine inabeba mzigo ulio sawa[3][4].

Kurusha hewani[hariri | hariri chanzo]

Ilijengwa na kampuni ya Stratolaunch Systems kwa kusudi la kubeba roketi zinazorushwa hewani na kulenga anga-nje. Mbinu huu unapunguza gharama kwa kurusha roketi kuanzia kimo cha mita 10,500.[5]

Jina[hariri | hariri chanzo]

Ilhali stratolaunch ni jina la kampuni, Roc ni kifupi cha "rocket carrier" na wakati huohuo mchezo wa neno maana katika fasihi ya Uarabuni na Ulaya ndege-dubwana Rok (pia Roc, Rokh au Rukh, ar. رُخّ rukh) alikuwa ndege mkubwa wa ajabu anbaye chakula chake kilikuwa tembo, pia aliweza kubeba jahazi pamoja na watu wake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Stratolaunch becomes world’s largest aircraft to fly, tovuti ya flightglobal ya 13 Aprili 2019
  2. Stratolaunch Aircraft Makes First Rollout To Begin Fueling Tests, tovuti ya stratolaunch.com, kupitia archive.org, 31 Mei 2017
  3. Stratolaunch Aircraft Makes First Rollout To Begin Fueling Tests, tovuti ya Stratolaunch inataja tani 250
  4. The Antonov Giants: An-22, An-124, & An-225, tovuti ya airvectors.net; Antonov inatajwa pia na uwezo wa kubeba tani 250
  5. Roketi inatumia kiasi kikubwa cha nishati kupaa kilomita za kwanza kwenye angahewa nzito; roketi inahitaji kubeba fueli pamoja na tangi ya oksijeni kwa ajili ya kuchoma fueli yake; ndege inabeba fueli pekee kwa sababu inachukua oksijeni hewani kwa hiyo inafika kimo cha kilomita 10 kwa gharama ndogo kwa kulinganisha na roketi.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: