Nenda kwa yaliyomo

Stethoskopu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Stethoskopu.
Matumizi ya stethoskopu.

Stethoskopu (kutoka Kiing. stethoscope) ni kifaa cha kusikilizia sauti zinazotoka katika viungo mbalimbali vya mwili kama vile moyo, mapafu au utumbo. Inatumiwa na matabibu na wafanyakazi wengine wa tiba kwa kuwekwa kwenye sehemu ya mwili iliyo karibu na viungo vinavyochunguzwa.

Stethoskopu ya kisasa imeundwa na bomba la plastiki linalonyumbulika lenye kifaa cha sikioni upande mmoja na kifaa cha kutambua sauti upande mwingine.

Kifaa cha kutambua sauti kina umbo la kengele inayofunikwa kwa utando mwembamba. Utando hutumiwa kusikiliza kifua cha mtu kwa sauti za juu. Umbo la kengele husaidia kutambua sauti za chini. Sauti za mapafu zina masafa ya juu kuliko sauti za moyo.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stethoskopu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.