Nenda kwa yaliyomo

Stéphanie Mbanzendore

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Stéphanie Mbanzendore ni mwanamke kutoka Burundi, ambaye amekaa Rotterdam nchini Uholanzi tangu mwaka 2003. Ni mwanzilishi wa shirika la Wanawake wa Burundi kwa ajili ya Amani na Maendeleo (BWPD). Pia ni mwenyekiti wa Mtandao wa wanawake wa tamaduni mbalimbali wapenda amani, na alishiriki kwenye shughuli mbalimbali za haki za wanawake na amani.

Stéphanie Mbanzendore alizaliwa na kukulia Burundi, ambapo baadae alipata elimu na kufanya kazi. Alifanya hivyo akiwa Rotterdam huko Uholanzi[1].

Mbanzendore ni mwanzilishi wa shirika la wanawake wa Burundi kwa ajili ya amani na maendeleo, yenye makao yake Uholanzi, ambapo alilenga wanawake na watu wa rika la vijana, pia yupo hai kwenye shughuli zinazohusu amani, kutatua migogoro na kuzuia maambukizi ya UKIMWI/VVU, mara nyingi ndani ya Burundi, lakini alifanya kushirikiana na wanawake wa nchini Rwanda na Kongo[2]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-21. Iliwekwa mnamo 2022-02-21.
  2. "Stephanie Mbanzendore". African Studies Centre Leiden (kwa Kiingereza). 2015-09-21. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-21. Iliwekwa mnamo 2022-02-21.