Nenda kwa yaliyomo

Spider-Man: Far From Home

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Spider-Man: Far From Home ni filamu iliyoachiliwa mwaka 2019 na kampuni ya kutengeneza filamu ya nchini Marekani iitwayo Marvel studios.

Filamu hii imeundwa kulingana na visa vilivyoandikwa kwenye vitabu vya hadithi vya Marvel. Marvel studios ikishirikiana na Columbia Pictures wameweza kutengeneza filamu hiyo huku ikisambazwa na Sony Pictures Releasing. Filamu hii ni mwendelezo wa filamu ya Spider-man: Homecoming (2017) na ni filamu ya ishirini na tatu toka kwa Marvel cinematic universe (MCU).

Filamu hii imeigizwa na Tom Holland kama Peter Parker/ Spider-Man akiwa kama mhusika mkuu akishirikiana na Samuel L. Jackson, Zendaya, Cobie Smulders, Jon Favreau, J. B. Smoove, Jacob Batalon, Martin Starr, Marisa Tomei, na Jake Gyllenhaal.

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Spider-Man: Far From Home kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.