Soucis Ya Likinga
Soucis Ya Likinga | |||||
---|---|---|---|---|---|
Studio album ya Pepe Kalle | |||||
Imetolewa | 1986 | ||||
Imerekodiwa | 1985-1986 | ||||
Aina | Soukous | ||||
Lebo | Kagi Production – KP 086 | ||||
Wendo wa albamu za Pepe Kalle | |||||
|
"Soucis Ya Likinga" ni albamu iliyotoka mwaka 1986 kutoka kwa msanii wa muziki wa soukous kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Pepe Kalle. Albamu ina nyimbo nne tu, mbili upande A na mbili upande B. Hii ni albamu ya kwanza ya Pepe Kalle kuitengeneza akiwa nchini Ufaransa. Katika albamu Pepe Kalle katunga nyimbo mbili tu—Soucis Ya Likinga na Dadou 2e Version. Wakati Perfusion ukiwa utunzi wake Misha Mfum na Simplicité imetungwa na Solo Sita.
Albamu ilisambazwa na Bade Stars Music – BSM 996.
Upande wa ufundi, Pepe Kalle ndiye aliyeipanga albamu nzima. Gitaa kuu lilipigwa na Kinanga Boeing 737 na Doris Ebuya, gitaa la kati Elvis Kunku — wakati waimbaji walikuwa akina Misha Mfum, Papa Djoss, Pépé Kallé na Solo Sita.
Orodha ya nyimbo
[hariri | hariri chanzo]Zifuatazo ni orodha kamili ya nyimbo zinapatikana katika albamu hii.
- A1 - Soucis Ya Likinga
- A2 - Perfusion
- B1 - Dadou 2e Version
- B2 - Simplicité
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Soucis Ya Likinga katika wavuti ya Discogs.