Nenda kwa yaliyomo

Jimbo la Sokoto

Majiranukta: 13°05′N 5°15′E / 13.083°N 5.250°E / 13.083; 5.250
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sokoto)
Jumba la Sultan, Sokoto
Jimbo la Sokoto
Jina lingine la Jimbo hili: Seat of Caliphate
Mahali
Location of Sokoto State nchini Nigeria
Takwimu
Gavana
(Orodha)
Aliyu Wamakko (PDP)
Tarehi lililoanzishwa 3 Februari 1976
Mji mkuu Sokoto
Eneo Eneo a eneo kilmota 25,973
liko katika nafasi ya 16
Idadi ya Watu
Sensa ya mwaka wa 1991
2005 est
Liko katika nafasi ya 14
4.392.391
4.244.399
GDP (PPP)
 -Jumla
 -Per capita
2007 (kadirio)
bilioni dola 4.82 [1]
dola 1.274 [1]
ISO 3166-2 NG-SO
Mahali pa jimbo la Sokoto katika Nigeria

Jimbo la Sokoto (lilianzishwa mwaka wa 1976) ni jimbo katika sehemu ya kaskazini-magharibi mwa Nigeria. Jimbo hili lilipata jina lake kutoka kwa mji wake mkuu wa Sokoto, mji ambao una historia ya muda mrefu na kiti cha Sokoto Caliphate.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tangu uanzishi wake kama jimbo mwaka wa 1976 (kutokana na kugawanywa kwa jimbo la kaskazini-magharibi kuwa majmbo mawili ya Sokoto na Niger, jimbo la Sokoto limetawalwa na magavana na maafisa wengi wa kijeshi wa zamani, kila mmoja wao akipata muda mfupil kutawala.

Sokoto, kama eneo, lina historia ndefu. Wakati wa utawala wa himaya ya Fulani katika karne ya 19, Sokoto lilikuwa jimbo muhimu la Fula na pia lilikuwa mji mkuu wa sehemu lililokuwa linajulikana kama magharibi ya kati ya Sudan.

Kutoka mwaka 1900 hivi, wakati Waingereza walianza ukoloni, Sokoto, ambayo ililkuwa inazunguka sehemu nzima ya kona ya kaskazini-magharibi ya Nigeria, ikawa mkoa wa "British protectorate" wa Nigeria. Hii haikuwa muda mrefu baada Gando kuongezwa kama mkoa mdogo wa Sokoto. Mikoa hii miwili kisha ilifunlika eneo a eneo maili elfu 35 (eneo a eneo kilomita elfu 90) na wakazi walikadiriwa kuwa zaidi ya laki 5. Mikoa hii ilijumuisha falme za Zamfara na Argunga, au Kebbi.

Ifuatayo kutoka Encyclopaedia Britannica ya mwaka wa 1911 inatoa baadhi ya taarifa kutoka mtazamo wa Waingereza waliokuwa katika utawala:

Mkoa umekuwa ukipangwa kwenye kanuni sawa kama za mikoa mingine ya Kaskazini mwa Nigeria. Mkazi wa Uingereza wa daraja la kwanza amewekwa katika sehemu ya Sokoto na wakazi wasaidizi wamewekwa katika vituo vingine. Mahakama ya Kiingereza ya haki yameanzishwa na magavana Waingereza wamegawanywa katika robo nne katika mkoa. Makundi ya polisi wa raia pia wamewekwa katika stesheni kuu. Nchi imetathminiwa kutumia mfumo mpya wa ushuru na inafunguliwa kwa haraka iwezekanavyo kwa ajili ya uuzaji. Baada ya uanzilishi wa utawala wa Kiingereza, wakulima na wafugaji waliingia katika wilaya na wenyeji wa miji walikusanyika na kurudi katika ardhi hiyo, kisha walijenga tena vijiji ambavyo vililkuwa vimewachwa kwa muda wa miaka hamsini. Ufugaji wa farasi na ngombe unafomu chanzo kuu cha mali katika mkoa huu. Kuna baadhi ya ukulima wa ndege ya aina ya Ostrich. Isipokuwa katika maeneo ya mchanga, kuna kilimo kwa upana, kama vile ukulima wa mchele na pamba. Mazao maalumu yanapandwa katika mabonde kwa njia umwagiliaji. Ushonaji, uwekaji wa rangi kwa vidude na mchakato wa kubadilisha ngozi kuwa ngozi laini ndizo viwanda kuu. Barabara nzuri ziko katika mchakato wa ujenzi mkoani. Uuzaji unaongezeka na fedha taslimu zimeanzishwa.
[...]
Mwaka wa 1906 mchipuko(rising) uliyotokana na mapenzi wa dini ilitokea karibu na Sokoto ambapo kwa bahati mbaya maafisa weupe watatu walipoteza maisha yao. Emir alimkana kiongozi wa mchipuko, ambaye alidai kuwa Mahdi aliyechochewa kuwafukuza wazungu nje ya nchi. Kikosi cha Kiingereza kiliandamana dhidi ya waasi, ambao waliondolewa na kupata hasara kubwa mnamo Machi mwaka wa 1906. Kiongozi alihukumiwa kifo katika mahakama ya Emir na kunyongwa katika mahali pa soko huko Sokoto, na tukio hilo lilikuwa la kuvutia hasa kuonysha uaminifu kwa utawala wa Kingereza ambao ulichochea pande zote kutoka watawala.

Mwaka wa 1967, si muda mrefu baada ya Nigeria kupata uhuru kutoka Uingereza, eneo hilo lilijulikana kama jimbo la Northwestern. Mwaka wa 1976, eneo hili liligawanywa katika majimbo mawili ya Sokoto na Niger. Baadaye, jimbo la Kebbi (1991) na jimbo la Zamfara (1996) zilijitoa katika jimbo la Sokoto.

Idadi ya watu

[hariri | hariri chanzo]

Jimbo la Sokoto lina hasa watu wa Kihausa. Wakazi wengi wa jimbo la Sokoto ni Waislamu wa Sunni, na wachache wakiwa waislamu wa Shia; ghasia kati ya makundi haya mawili ni ya kawaida.

Hali ya hewa

[hariri | hariri chanzo]

Jimbo la Sokoto liko katika Sahel kavu, na limezungukwa na savannah ya mchanga na milima .

Likiwa na wastani wa joto wa nyuzi 28.3, Sokoto ni eneo la joto jingi sana. Hata hivyo, upeo wa joto wa mchana kwa wakati mwingi wa mwaka huwa chini ya digri 40 kwa ujumla na ukavu huu hufanya joto usiwe wa kufurahisha. Miezi ambayo ina joto huanzia Februari hadi Aprili wakati joto wa mchana unaweza kuzidi nyuzi 45. Msimu wa mvua ni kuanzia Juni hadi Oktoba wakati ambao mvua kunyesha ni tukio kila siku. Mvua, nadra hukawia muda mrefu sana na ni tofauti sana na mvua ya kawaida mvua inayojulikana katika maeneno ya kitropiki. Kuanzia mwisho wa Oktoba hadi Februari, wakati wa msimu wa baridi , hali ya hewa huwa limejaa upepo wa Harmattan unaovuma vumbi wa Sahara juu ya ardhi. Vumbi hupunguza mwangaza na hivyo basi hupunguza joto maradufu na kupelekea shida ya vumbi katika kila sehemu ya nymba.

Kupandwa kwa mazao katika eneo hili hutegemea tambarare za mafuriko za mfumo wa mto wa Sokoto-Rima (angalia mto wa Sokoto), ambazo zimefunikwa na udongo tajiri wa aina ya "alluvial". Ukavu wa eneo kwa jumla hurusu mazao chache, labda mtama huwa kwa wingi, pamoja na mchele, mahindi, maharage na nafaka nyinginezo. Mbali na nyanya, mboga chache hukua katika eneo. Kutopatikana kwa aina mbalimbali ya vyakula kumesababisha vyakula chache vilivyopikwa vya mtaa .

Maeneo ya Serikali za Mitaa

[hariri | hariri chanzo]

Maeneo 23 ya Serikali za Mitaa ya Sokoto ni:

  1. Binji
  2. Bodinga
  3. Dange Shuni
  4. Gada
  5. Goronyo
  6. Gudu
  7. Gwadabawa
  8. Illela
  9. Isa
  10. Kebbe
  11. Kware
  12. Rabah
  13. Sabon Birni
  14. Shagari
  15. Silame
  16. Sokoto Kaskazini
  17. Sokoto Kusini
  18. Tambuwal
  19. Tangaza
  20. Tureta
  21. Wamako
  22. Wurno
  23. Yabo
  1. 1.0 1.1 "C-GIDD (Canback Global Income Distribution Database)". Canback Dangel. Iliwekwa mnamo 2008-08-20.
  • Nigeria [map]. Collins Bartholomew Ltd 2005. Published by Spectrum books Ltd

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]


 
Majimbo ya Nigeria
Abia | Abuja Federal Capital Territory | Adamawa | Akwa Ibom | Anambra | Bauchi | Bayelsa | Benue | Borno | Cross River | Delta | Ebonyi | Edo | Ekiti | Enugu | Gombe | Imo | Jigawa | Kaduna | Kano | Katsina | Kebbi | Kogi | Kwara | Lagos | Nasarawa | Niger | Ogun | Ondo | Osun | Oyo | Plateau | Rivers | Sokoto | Taraba | Yobe | Zamfara

13°05′N 5°15′E / 13.083°N 5.250°E / 13.083; 5.250

Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jimbo la Sokoto kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.