Nenda kwa yaliyomo

Simon Msuva

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simon Msuva
Maelezo binafsi
Jina kamili Simon Happygod Msuva
Tarehe ya kuzaliwa 3 Desemba 1993 (1993-12-03) (umri 31)
Mahala pa kuzaliwa    Dar es Salaam, Tanzania
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Al Jadida
Namba 27

* Magoli alioshinda

Simon Happygod Msuva (alizaliwa 3 Desemba 1993 jijini Dar es Salaam, Tanzania) ni mchezaji wa kandanda ambaye anacheza nafasi ya winga mshambuliaji katika timu ya Al Jadida kutoka nchini Moroko .

Msuva ni mfungaji bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2014-2015: Alifunga magoli kumi na saba. Mwaka 2016-2017 aliibuka tena mfungaji bora akiwa na magoli kumi na nne. Pia alikuwa mfungaji bora katika Kombe la Mapinduzi lililofanyika mwaka 2015 akifunga magoli manne.

Bwana Msuva amewahi kufanyiwa majaribio katika klabu inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini ambayo ni Bidvest na majaribio hayo akaweza kufanikiwa lakini kilabu yake ya Young Africans Sc waligoma kumuuza winga huyu kutokana na makubaliano na timu hiyo.

Mwanzoni mwa mwaka wa 2017 aliingia mkataba kuchezea na klabu ya Al Jadida ya nchini Moroko.

Timu alizowahi kuchezea

Azam FC 2010-2011 Moro United 2011-2012 Young Africans SC 2012-2017

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Simon Msuva kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.