Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Shaheed Minar, au kumbukumbu la mashahidi, kwenye Chuo Kikuu cha Dhaka, Bangladesh, inayofanya ukumbusho wa wanafunzi waliokufa kwa ajili ya lugha ya Bangla tarehe 21 Februari 1952

Tarehe 21 Februari imetangazwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama na UNESCO tarehe 17 Novemba 1999. Tangu tarehe ile imetambuliwa pia na Umoja wa Mataifa katika azimio lake la 16 Mei 2007, lililotangaza mwaka wa 2008 kuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa.[1]

Asili ya Siku ya Lugha ya Mama ni tukio la mwaka wa 1952 nchini Bangladesh, wanafunzi wa chuo kikuu wa Dhaka walipofanya maandamano kwa ajili ya lugha ya Bangla, na wengine wao kuuawa na polisi kwa kupigwa risasi.

Siku ya Lugha ya Mama husherehekewa kila mwaka tangu mwaka wa 2000 na nchi zilizojiunga na UNESCO, kwa ajili ya kujadili mambo ya wingi wa lugha, haki za lugha zote, na mazingira ya kutumia lugha tofauti.

Mada za kila mwaka[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida, Siku ya Lugha ya Mama ina mada tofauti kila mwaka.[2]

  • 2000, Sherehe ya kwanza
  • 2001, Sherehe ya pili
  • 2002, Wingi wa lugha: lugha elfu tatu ziko hatarini kufa
  • 2003, Sherehe ya nne
  • 2004, Elimu ya watoto[3])
  • 2005, Lugha kwa wasioona na kwa wasionena
  • 2006, Lugha na Mtandao
  • 2007, Elimu kwa lugha nyingi
  • 2008, Mwaka wa Lugha wa Kimataifa

Matukio mengine[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Ona pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.