Shiraz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shiraz شیراز
Boma la Karim Khan, Shiraz
Nchi Uajemi (Iran)
Jimbo / Mkoa Fars
Anwani ya kijiografia Coordinates: 29°37′N 52°32′E / 29.617°N 52.533°E / 29.617; 52.533
Eneo km² 240
Wakazi 1,565,572
Msongamano wa watu 6670/km²
Simu 071
Tovuti rasmi www.shiraz.ir

Shiraz ni mji mkubwa na muhimu nchini Uajemi (Iran). Ni jiji lenye watu milioni 1.4 hivi na mji mkuu wa eneo la Farsi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jina la Shiraz linaonekana tayari kwenye vigae vya mwandiko wa kikabari vilivyokutwa katika maghofu ya Persepolis.

Wakati wa uvamizi wa Waarabu Waislamu mnamo mwaka 650 BK mji ilikuwa kitovu cha Uajemi kusini.

Mnamo mwaka 1000 Shiraz ilikuwa mji mkuu wa nasaba ya Wabuya waliotawala sehemu kubwa za Iran na Irak pamoja na pwani ya Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf). Katika kipindi hiki iko pia asili ya masimulizi kuhusu "Washirazi" waliosemekana kutoka "Shiraz" na kukimbilia pwani ya Afrika ya Mashariki.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Shiraz kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.