Shinagimbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shinagimbi ni sehemu fupi ya chini ya shina la mimea fulani iliyovimba chini ya ardhi na kutumika kama ogani ya kuhifadhi chakula (wanga) ambayo mimea hiyo hutumia kuishi wakati wa baridi au hali nyingine mbaya kama ukame na joto. Mifano ni mgomba, magimbi, myugwa, uwanga na spishi za Alocasia, Sagittaria, Xanthosoma na mingi mingine.

Tofauti na kiazi ni kwamba hicho ni sehemu ya mzizi. Na tofauti na tunguu ni kwamba hilo lina majani mengi manene kama magamba.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shinagimbi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.