Serah Ndanu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Serah Ndanu Teshna (maarufu kwa jina la Serah Ndanu; amezaliwa 3 Machi 1988) ni mwigizaji kutoka Kenya.[1]

Ni mmoja wa waigizaji kutoka Kenya mwenye umaarufu kutokana na kazi zake za uigizaji na uongozaji wa vipindi vya televisheni.[2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Ndanu alionekana katika filamu nyingi maarufu moja wapo ni The Rugged Priest mwaka 2011. Kutokana na utendaji bora, alinyakua tuzo ya muigizaji bora wa kike ya mwaka 2011 maarufu kwa jina la Kalasha Awards.[3] Mwaka 2013, alikua mhusika katika filamu ya Kiswahili kwa jina la, Sumu la penzi, pamoja na Avril, Naomi Ng'ang'a na Joyce Maina. Kazi yake ya siku za karibuni ni uhusika wa Trizzy katika tamthiliya ya Sue na Johnnie inayoonyeshwa Maisha Magic East [4]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Kazi Uhusika Maelezo
Televisheni/Filamu
2010-2013 Noose of Gold Soila Mhusika mkuu
2010 Nairobi Law Mshiriki
2011 The Rugged Priest Alice Mhusika mkuu; Filamu
2013–mpaka sasa Sumu la penzi Miriam Mhusika mkuu
2015–mpaka sasa The Skin Therapy Show Mwenyewe Mtayarishaji
2016–mpaka sasa Twisted Billy Mhusika mkuu

Tuzo na Uteuzi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Chuo Tuzo Kichwa Matokeo marejeo
2011 Kalasha Awards Muigizaji Bora wa kike The Rugged Priest Kigezo:Mshindi [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Serah Ndanu biography. Iliwekwa mnamo October 11, 2015.
  2. In the cottage with Serah Ndanu. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-12-22. Iliwekwa mnamo October 29, 2015.
  3. 3.0 3.1 2011 Kalasha Awards. Iliwekwa mnamo October 29, 2015.
  4. Serah Ndanu takes no prisoner. Iliwekwa mnamo October 29, 2015.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Serah Ndanu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.