Nenda kwa yaliyomo

Seneta worldwide

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jackson Daudi Mukangara (maarufu kama Seneta Worldwide, alizaliwa 16 Desemba 1987 nchini Tanzania) Ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea nchini Tanzania na pia ni mtunzi wa mashairi.

Amefanikiwa kujizolea umaarufu mara tu baada ya kuonyesha nyota yake mnamo mwaka 2002 baada ya kutoa wimbo wake wa kwanza uitwao Pili na Lili na kufanya nyimbo hii kumtambulisha katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava.

Elimu na maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Seneta Worldwide alisoma shule ya msingi Mlimani iliyopo jiini Dar es Salaam kuanzia darasa la awali mpaka kufikia kuhitimu darasa la saba na kisha kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Shaaban Robert iliyopo jijini Dar es salaam na kwenda kumalizia elimu yake ya sekondari nchini kenya katika shule ya sekondari Peponi School. Pia akiwa huko nchini kenya alipata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu katika chuo cha United States International University na kuweza kuhitimu na kutunukiwa Shahada ya kwanza ya biashara.

akiwa bado anaishi huko nchini kenya ndoto zake za kuwa mwanamuziki zilianzia huko nchini Kenya taratibu kabla ya kuanza safari ya maisha yake ya muziki rasmi nchini Tanzania.

Shughuli za Muziki

[hariri | hariri chanzo]

Jackson Daudi Mukangara au maarufu kwa jina la Seneta Worldwide nyota huyu wa Bongo Flava alizidi kujipatia umaarufu wake pale alipopata nafasi ya kuimba kwenye uzinduzi wa Album ya Mr II (Sugu) katika ukumbi wa Diamond Jubilee Desemba 24, 2009 jijini Dar es Salaam (kwenye Mkesha wa Krismasi).

Baada ya kujipatia mashabiki mbalimbali nchini Tanzania hapa ndipo kipaji chake kiliweza kuonekana zaidi kwa kuonyesha uwezo wake mahiri wa kutoa burudani kwa mashabiki nchini Tanzania.

Aliweza kukubalika na kufanikiwa kwenye muziki wa Bongo Flava kwa uwezo wake wa kuimba nyimbo mbalimbali na uwezo huo ulifika hatua ya kuweza kushirikiana na baadhi ya wasanii wa nchini Tanzania kama vile Country boy, Mr Blue Byser, Foby, King Zilla. [1][2]

katika harakati zake za muziki msanii Seneta Worldwide alishawahi kuachia wimbo uliofanya vizuri sana Tanzania na hatimaye kuweza kuvuka mipaka hadi kufikia nchini Kenya alipokuwa akifanya masomo yake kwa miaka kadhaa na kuweza kuongeza mashabiki kwenye nchi hii ya jirani na Tanzania, wimbo huo uitwao Andazi aliutoa mnamo mwaka 2010.[3]

Katika safari yake ya muziki nchini Tanzania msanii Seneta Worldwide anayeimba muziki wake kwa style ya Bongo Flava alishaitwa na kushiriki kwenye matamasha makubwa nchini Tanzania kama vile FIESTA ya mwaka 2012 tamasha ambalo linaandaliwa na Clouds Fm na pia kwa tamasha la BARKWABAR linaloandaliwa na kituo cha redio cha EFM.[4]

Hivyo hivyo alishawai pia kushinda tuzo ya msanii bora akiwa masomoni Kenya (Best Pop Idol).

  1. Seneta Seneta Ft Country boy & Foby - Bata, iliwekwa mnamo 2023-02-02
  2. Seneta Worldwide feat Mr Blue - MANUA (Official Music Video), iliwekwa mnamo 2023-02-02
  3. andazi.mp4, iliwekwa mnamo 2023-02-02
  4. @senetaworldwidePERFORMS LIVE #efm #BAKWABAR CONCERT #DAR ES SALAAM #TANZANIA #BUNJU @EDigitalTanzania, iliwekwa mnamo 2023-02-02

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

https://web.facebook.com/KissFmTanzania/videos/kmw/627363191820683/?_rdc=1&_rdr

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Seneta worldwide kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.