Fyekeo
Fyekeo[1] (kutoka kitenzi "kufyeka"; kwa Kiingereza scythe) ni zana ya kilimo kwa ajili ya kukata nyasi au nafaka kama ngano. Muundo wake unafanana na mundu lakini kisu na mpini ni mrefu zaidi. Zinamwezesha mtumiaji kukata eneo kubwa kwa urahisi kulinganishwa na matumizi ya mundu au kifyekeo cha kawaida.
Mtumiaji wake anasimama wakati anakata nyasi. Kisu kinahitaji kunolewa mara kwa mara, hivyo kila mtumiaji hubeba pia jiwe la kunoa.
Fyekeo ilikuwa kifaa kikuu cha kukata nyasi na kuvuna nafaka katika Ulaya, Asia ya Magharibi na Marekani hadi kusambaa kwa mashine zinazotekeleza shughuli hizo. Fyekeo zinatumiwa bado, hasa katika mazingira ambako tabia ya uso wa ardhi hairuhusu matumizi ya mashine.
Katika Afrika matumizi ya fyekeo hayajaenea; inasemekana mara nyingi nyasi za Afrika ni ngumu mno kwa zana hiyo. Hata hivyo kuna majaribio ya kufundisha matumizi yake kwa wakulima wadogo wasio na uwezo wa kugharamia mashine.
Katika Kiswahili neno fyekeo linatumika zaidi kumaanisha "kwanja".
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Simon Fairlie: Notes on the History of the Scythe and its Manufacture Ilihifadhiwa 7 Mei 2021 kwenye Wayback Machine., tovuti ya Scythe Association, Uingereza.
- Sjoerd W. Duiker: Mowing with Scythes, tovuti ya Smallfarmerjournal.org, Vol. 37, No. 2 – Spring 2013
Video
[hariri | hariri chanzo]- Scythe mowing in East Africa, filamu kuhusu programu ya Chuo kikuu cha Penn State nchini Kenya, mwaka 2012
- Scythe Project in India 2016 (filamu kuhusu kufundisha fyekeo katika mazingira walipovuna kwa mundu)