Mjusi-islam
Mandhari
(Elekezwa kutoka Scincidae)
Mjusi-islam | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Jozi ya magonda mdomo-vidoa wakipandana (Trachylepis maculilabris)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nusufamilia 3:
|
Mijusi-islam ni mijusi wa familia Scincidae walio na ngozi laini inayong'aa. Spishi za jenasi Trachylepis huitwa magonda pia. Miguu ya mijusi hawa ni mifupi kwa kawaida na spishi nyingi zina miguu iliyopunguka au hazina miguu. Spishi hizi husongea kama nyoka.
Mijusi hawa ni wafupi (sm 5-6) hadi warefu kiasi (sm 60). Huishi kati ya mawe na miamba, katika vishimo, chini ya mchanga au takataka ya majani au juu ya miti. Chakula chao ni wadudu hasa lakini nyungunyungu, majongoo, konokono, mijusi wengine au vipanya pia.
Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Acontias percivali, Mjusi Bila-miguu wa Percival (Perciavl's legless skink)
- Chalcides ocellatus, Mjusi Madoa-macho (Ocellated skink)
- Leptosiaphos kilimensis, Mjusi Vidole-vitano wa Kilimanjaro (Kilimanjaro five-toed skink)
- Lygosoma pembanum, Mjusi-finginyika wa Pemba (Pemba Island writhing skink)
- Melanoseps loveridgei, Mjusi Bila-miguu wa Loveridge (Loveridge's limbless skink)
- Mochlus afer, Mjusi-finginyika Mweusi (Peters's writhing skink)
- Panaspis wahlbergi, Mjusi Bila-kope Savana (Wahlberg's snake-eyed skink)
- Scelotes uluguruensis, Mjusi Mchimbaji wa Uluguru (Uluguru fossorial skink)
- Trachylepis brevicollis, Gonda Shingo-fupi (Short-necked skink)
- Trachylepis maculilabris, Gonda Mdomo-vidoa (Speckle-lipped skink)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mjusi bila-miguu wa Percival
-
Mjusi madoa-macho
-
Mjusi-finginyika wa Sundevall
-
Mjusi mchimbaji mdogo wa Msumbiji
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mjusi-islam kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |