Sanamu kubwa za Amenhotep III na Tiye

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu kubwa ya Amenhotep III na mke wake.

Sanamu kubwa za Amenhotep III na Tiye ni kundi la sanamu za mawe za farao wa zamani wa Misri Amenhotep III wa nasaba ya kumi na nane ya Misri, mke wake Tiye na mabinti wao watatu.

Muunganiko wa sanamu hizo huunda kiu kikubwa zaidi kilichowahi kuchongwa katika historia.[1] Awali, sanamu hizo zilisimama kwenye hekalu la Medinet Habu, Magharibi mwa Thebes; leo hii zipo katikati ya ukumbi mkubwa wa Makumbusho ya Misri mjini Cairo.

Muonekano[hariri | hariri chanzo]

Sanamu hizo zimetengenezwa kwa chokaa, upana wake ni mita 4.4 na kimo chake ni mita 7. Macho yake yana umbo la mlozi na nyusi zake zimepinda, kiashirio cha nasaba ya kumi na nane ya Misri.[2][3]

Sanamu hizo zikiwa Kwenye Ukumbi wa Makumbusho.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. W. Raymond Johnson: Monuments and Monumental Art under Amenhotep III. In: Amenhotep III: Perspectives on His Reign. (edited by David O'Connor, Eric H. Cline) p.73
  2. Abeer El-Shahawy: The Egyptian Museum in Cairo. American Univ in Cairo Press, 2005, p.183, ISBN|9789771721833
  3. Chief of Seers: Egyptian Studies in Memory of Cyril Aldred. (ed. Elizabeth Goring, Nicholas Reeves, John Ruffle). Routledge & National Museums of Scotland, Edinburgh, 2009, p.69, ISBN|978-0-7103-0449-0
Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sanamu kubwa za Amenhotep III na Tiye kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.