Sala ya mchana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sala ya mchana katika "Liturujia ya vipindi" ni sala rasmi iliyopangwa kwa saa za mchana kati ya Masifu ya asubuhi na Masifu ya jioni.

Imegawanyika katika vipindi vitatu vifupi: Kabla ya adhuhuri, Adhuhuri na Baada ya adhuhuri.

Vipindi hivyo vinatokana na desturi ya Uyahudi iliyoendelea kufuatwa na Wakristo, inavyoshuhudiwa na kitabu cha Matendo ya Mitume.

Kati ya utangulizi na baraka ya mwisho, sala hiyo inaundwa na utenzi, Zaburi tatu au vipande vitatu vya Zaburi moja ndefu, somo fupi kutoka vitabu vingine vya Biblia ya Kikristo, kiitikizano kifupi na sala ya kumalizia.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sala ya mchana kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.