Nenda kwa yaliyomo

Saidi (nyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Saidi)
Saidi
(Beta Pegasi, Scheat)
Kundinyota Farasi (Pegasus)
Mwangaza unaonekana 2.4 (geugeu 2.3 – 2.7)[1]
Kundi la spektra M2 II-III
Paralaksi (mas) 16.64 ± 0.15
Umbali (miakanuru) 196
Mwangaza halisi -1.4
Masi M☉ 2.1
Nusukipenyo R☉ 95
Jotoridi usoni wa nyota (K) 3689
Majina mbadala 53 Peg, HR 8775, BD +27°4480, HD 217906, SAO 90981, FK5 870, HIP 113881.


Saidi (lat. & ing. Scheat pia β Beta Pegasi [2], kifupi Beta Peg’’’, β Peg’’’) ni kati ya nyota angavu za kundinyota ya Farasi (Pegasus).

Jina la Saidi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [3]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema kwa kawaida الساعد as-sa’id inayomaanisha “mkono" (au mguu wa farasi). Walitafsiri kwa njia hii maelezo ya Ptolemaio asiyetumia jina lakini alieleza “nyota kwenye mbega wa kulia pale ambako mguu unaanza”. [4]

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu kwa tahajia ya Kijerumani jinsi ilivyokuwa kawaida katika Ulaya na kuorodhesha nyota kwa jina la "Scheat" [5] .

Beta Pegasi ni jina la Bayer ; Beta ni herufi ya pili katika Alfabeti ya Kigiriki na Saidi ni nyota angavu ya pili katika Farasi - Pegasus.

Saidi ni nyota jitu jekundu katika kundi la spektra M2 ikiwa umbali wa karibu miaka nuru 200. Ni pia nyota badilifu ni mwangaza wake unacheza baina ya mag 2.3 na 2.7 kila baada ya siku 41.

  1. vipimo kufuatana na (2009)
  2. Pegasi ni uhusika milikishi (en:genitive) wa "Pegasus" katika lugha ya Kilatini na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa, Beta, Beta Pegasi, nk.
  3. ling. Knappert 1993
  4. Toomer (1984), Almagest, uk 358, XIX 3
  5. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Mauron, N.; Caux, E. (November 1992), "K I/Na I scattering observations in circumstellar envelopes - Alpha(1) Herculis, Omicron Ceti, TX PISCIUM and Beta Pegasi", Astronomy and Astrophysics, 265 (2): 711–725,online hapa
  • Scheat katika Bright Star Catalogue online hapa
  • Ptolemy's Almagest, translated and annotated by G.J. Toomer, London 1984, ISBN 0-7156-1588-2 online hapa